WIZARA YA ELIMU YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO ILI KUPOKEA NA KUJADILI MAONI JUU YA RASIMU YA SERA YA MAFUNZO


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Kwa mara nyingine Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekutana na Wadau wa Maendeleo  jijini Dar es Salaam kuwapitisha, kujadili na kupokea maoni juu ya Rasimu ya Sera na mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 na Rasimu ya  Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu.


Akizungumza katika kikao kazi hicho, Waziri wa Elimu Mhe. Prof. Adolf  Mkenda amesema Wizara itaendelea kushirikiana na wadau hao katika kuhakikisha mageuzi ya elimu yanayofanyika yanafanikiwa.

"Mageuzi haya tunayofanya yanahitaji rasilimali katika kuyafanikisha, tuendelee kushirikiana ili yaweza kufanikiwa nasi tutaendelea kuwashirikisha katika kila hatua”,amesema Prof. Mkenda


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Carolyne Nombo amewashukuru wadau hao kwa namna  wanavyoendelea kufadhili miradi ya elimu yenye lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.


Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo ya Elimu ambae pia ni Mkuu wa Sekta ya Elimu  UNESCO Faith Shayo ameipongeza Serikali kwa mageuzi makubwa yanayofanyika kwenye elimu huku akiishukuru Wizara kwa kuwashirikia katika hatua mbalimbali kuelekea mageuzi hayo.



Previous Post Next Post