KITUO KIPYA CHA MAFUTA KILICHOJEGWA NA SUMA JKT KUANZA KUFANYA KAZI HIVI KARIBUNI


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia kwa Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali ,Hassan Mabena,amesema kupitia Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa (SUMA JKT)  litaendelea kuanzisha miradi mbalimbali kwa lengo la kuongeza mapato katika jeshi hilo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali ,Hassan Mabena, wakati akiweka jiwe la msingi katika kituo cha mafuta kilichopo kawe jijini Dar es Salaam ambapo kituo hicho kimejengwa na SUMA JKT.

Aidha,Brigedia Jenerali ,Mabena,amesema nia ya JKT kuwa na vyanzo vya mapato ambavyo vitasaidia katika kujikwamua.


"Adhima ya JKT na shirika lake ni kuwa miradi mipya kama fursa inavyojitokeza ile kuongeza kipato,natoa wito kwa shirika kuongeza miradi ya vituo vya mafuta katika mikoa mbalimbali"Amesema.Brigedia Jenerali ,Mabena

Hata hivyo,Brigedia Jenerali ,Mabena,amesema hatua ya ujenzi wa kituo hicho imetokana na utunzaji mzuri wa mapato na umechangia kuhakikisha ujenzi wake.

,Brigedia Jenerali ,Mabena,ameipongeza serikali,mashirika binafsi kwa kuendelea kuipa tenda mbalimbali SUMA JKT na kufanikiwa na kupata mapato ambayo yamepelekea kujengwa kwa kituo cha mafuta.


Kwa Upande wake,Leteni Kanali Lucy Batakanwa ambaye ni mkurugenzi mtendaji mwendeshaji wa SUMA logistic ,amesema mradi wa kituo cha mafuta ulianza mwezi wa nne wa mwaka jana na ujenzi wake umefikia asilimia 99.

"Kituo hichi kina matenki yenye kujaza lita elfu sabini,na pia katika katika kituo hicho kuna mashine ya kisasa"Amesema Luteni kanali Batakanwa.

Naye,Kaimu mkurugenzi mtendaji Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa (SUMA JKT),Kanali Shija Rupi,amesema mradi wa kituo hicho cha mafuta kimeghalimu zaidi ya milioni 883 na kubainisha zitawanufaisha wananchi wa eneo hilo.
Previous Post Next Post