SHIRIKA LA CATHOLIC RELIEF SERVICES LA SHEREKEA MIAKA 60 TANGU KUWEPO KWAKE TANZANIA


Lilian Ekonga

Shirika la Catholic Relief Services ( CRS) ambao ni wakala rasmi wa kimataifa wa kibinadamu wa jumuiya ya Kikatoliki nchini Marekani linasherekwa kutimiza miako 60 tangu kuwepo kwake nchini Tanzania. 

Akizungumza na waandishi wa Habari katika hafla ya kuazimisha miaka 60 jijiniDar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa CRS Sean Callahan amesema tangu mwaka 1962 CRS imekuwa ikihudumia jumuiya za Kitanzania kwa kujikita zaidi kupunguza umasikini na kutoa msaada kwa watu wanaohitaji msaada katika zaidi ya 100.

"Wakati CRS duniani inatimiza miaka80, ni heshima kubwa kuwapo Tanzaniakwamiaka 60, tukifanya kazi bega kwa bega na Kanisa Katoliki, washirika wetuwa maendeleona jumuiya tunazohudumia, na kazi hii inaendeleakuwa jukumu kubwakwetukutokana na uaminifu tuliopewa." amesema callahan. 

Ameongeza kuwa CRS imekuwa ikiunga mkono mabadiliko yanayochochewa na jamii kwa kiwango
kikubwa nchini kwa kufanya kazi bega kwa bega na viongozi wa dini mbalimbali, washirika wa kitaifa na jamii mbalimbali katika njia yao ya ustawi na ustahimilivu dhidi ya athari mbaya za changamoto kuu za leo, ikiwa ni pamoja na masuala ya jinsia, upatikanaji wa masoko na fedha kwa vijana, uhaba wa chakula na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa upande wake Katibu wa Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania Pardi Charlse kitima ameiomba serikali ya Tanzania kushirikiana na shirika la CRS kwa kuwa karibu kabisa maana wanachohakikisha kuwa huduma zao haziendi kidini zinaenda kumwangalia wanayemlenga kwa mipango yao ya maendeleo.


"Sasa hivi wamechukua maeneo muhimu afya na Kilimo kwaajili ya kuimarisha vijana kujiajiri kwenye sekta ya kilimo, Eneo la Lishe kuhakikisha vijana wanapata lishe nzuri ,eneo la elimu na maeneo mengine muhimu. amesema Pardi Kitima. 

Nae Mmoja ya wafanyakazi wa shirika la CRS Mary Mshota amesema wana miradi katika sekta kilimo , maji pamoja na afya makuzi na malezi kwa watoto wadogo, kupunguza udumavu hasa kanda ya kaskazini miradi ya lishe na kusapoti serikali kipindi cha Covid kuhamasisha maswala ya kupata chanjo na kujichanja.

"Kwa upande wa malez ya watoto CRS tunaangalia zaidi malezi na makuzi kwa mtoto kabla ya kuzaliwa ni jinsi gani wanaweza kuwasiliana na yule mtoto. Kwa kujenga akili ya mtoto kufikiria vizuri na ubongo uweze kufanya kazi vizuri" amesema mary.
Previous Post Next Post