HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA YAENDESHA ELIMU YA UHIFADHI, WANAKIJIJI WASALIMISHA SILAHA

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Kamanda Godwel Ole Meing'ataki (kulia) akipokea silaha aina ya gobole kutoka kwa mkazi wa Kijiji cha Matalawe Kata ya Mlowa  Jimbo la Isimani (shati la njano) aliyekabidhi baada ya kupata elimu ya ujirani mwema

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Kamanda Godwel Ole Meing'ataki (katikati), mkazi wa Kata ya Mlowa (kulia)  aliyekabidhi silaha hiyo baada ya kupata elimu ya ujirani mwema. Kushoto ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kata ya Mlowa (OCS), Eric Kabigumila

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kata ya Mlowa (OCS), Eric Kabigumila akiwa na silaha tatu aina ya gobole ambazo zimesalimishwa na Wanakijiji kufuatia elimu ya ujirani mwema


NA MWANDISHI WETU,
ISIMANI, IRINGA.


HIFADHI ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa ambayo ni miongoni mwa hifadhi kubwa nchini, kupitia Mkuu wa hifadhi hiyo, Kamanda Godwel Ole Meing'ataki na Kamati ya Ulinzi na Usalama, wameendelea na zoezi la kutoa elimu ya uhifadhi ikiwemo kupambana na ujangili kuzunguka Vijiji jirani na Hifadhi hiyo ambapo silaha zaidi ya zimeendelea kusalimishwa.


Awali Mkazi wa Kijiji cha Matalawe Kata ya Mlowa Jimbo la Isimani amekabidhi silaha yake aina ya Gobole kwa Mhifadhi Mkuu wa Ruaha,

Mkazi huyo amesema ameamua kusalimisha silaha hiyo aliyokuwa anaitumia Kwa ujangili wa kuwindia wanyama wa porini baada ya kupata elimu ya ujirani mwema.

Mbali na silaha hiyo ya Mkazi wa kijji cha Matalawe, pia alibadhiwa silaha zingine tatu zilizopokelewa na kukabidhiwa kwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kata ya Mlowa (OCS), Eric Kabigumila katika zoezi hilo kwa ushirikiano na Hifadhi hiyo ya Ruaha.

Zoezi la wananchi mbalimbali kusalimisha silaha zao kwa uwazi au kificho limeongezeka baada ya elimu inayoendelea kutolewa na Mkuu huyo wa hifadhi hada kwenye vijiji vinavyoizunguka hifadhi ya taifa Ruaha

Aidha, Meing'ataki amesema ameamua kusimamia zoezi la kutoa elimu ya uhifadhi Kwa wananchi baada ya kuona hali ya ujangili inaongezeka

Hadi sasa vijiji vilivyo tembelewa na kupewa elimu ya uhifadhi ni pamoja na Kijiji Cha Kisilwa, Mahuninga, Makifu, Mapogoro, Idodi, Matalawe pamoja na kijiji Cha Tungamalenga ambacho ndicho kinachoongoza Kwa ujangili Kwa mujibu wa tafiti.

Meing'ataki amesisitiza ni jukumu la Kila mwananchi kujua umuhimu wa kulinda na kuhifadhi urithi tuliopewa na Mungu Ili tuweke kuwarithisha watoto na wajukuu wetu kama ilivyo kauli mbiu ya uhifadhi isemayo "Tumerithishwa, tuwarithishe".
Previous Post Next Post