TAASISI YA AL-HIKMA YAKOSHWA NA UTENDAJI KAZI WA RAIS SAMIA HUSUSANI SEKTA YA ELIMU NCHINI


Na Lilian Ekonga. Jijin Dar es salaam

Uongozi wa shule ya kislam ya Alhkima umempongeza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan  pamoja na Wizara ya Elimu kwa kuongezeka kwa kiwango cha ufalu kwa wanafunzi wa kidato cha nne walio hitimu mwaka 2022.

Hayo yamesemwa leo januari 4 na  Mkurugenzi wa Al Hikma Foundation, Sheikh Nurdin Kishki katika Halfla ya kuwapongeza  wanafunzi waliofaulu vizuri katika matokeo yao kidato cha nne ndani ya shule zao za  sekondari ya  alhkima ya wanawake pamoja na wanaume jijini Dar es salaaam.


Ambapo amesema Katika Matokeo ya kidato cha nne shule ya alhkima ya wanaume iliweza kushika nafasi ya pili katika shule ya kislamu Tanzania zilizofanya vizuri kwa matokea ya kidato cha nne ya  mwaka 2022.

"Katika shule zote hakuna mwanafunzi aliyepata divisioni zero wala four, na kwa upande wa alhkima ya wanawake wanafunzi 26 walipata division 1, wanafunzi 44 walipata divison 2 na wanafunzi 1 alipata divisioni 3 na kwa  shule ya alhkima  ya wanaume wanafunzi 61 walipata division 1 na wanafunzi 18 walipata division 2," amesema shekh Kishki


Pia amewashukuru na kuwaponge  walimu wa shuleni hapo kwa jitihada zao kubwa za kuwafundisha wanafunzi hao na kuleta matokeo mazuri.

Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Temeke ,Abdul Buheti ametoa rai kwa wanafunzi hao waliofahuru vizuri kuhakikisha wanaenda kwenye shule za sekondari za serikali kwa kidato cha tano watakazo pangiwa ili wawe chachu ya  kuwafunza wanafunzi wengine maadili mazuri waliopata shuleni hapo hasa kwa upande wa dini. 


"Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania  Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya Bilioni 4 kwaajili ya ujenzi wa Madarasa 207 ya shule za sekondari Wilaya ya Temeke,"amesema Buheti.
Previous Post Next Post