NSOKOLO: RAIS SAMIA ATOA MATUMAINI YA KUFANYIWA MAREJEO YA SHERIA YA HABARI


Na Humphrey Msechu

Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani amekuwa ni rafiki wa waandishi wa habari, hayo yamesemwa na Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Deogratius Nsokolo

Akizungumza wakati akitoa maoni yake kuhusu mwenendo wa mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari nchini, ameeleza maendeleo ya mchakato huo yanatokana na kuridhiwa na Serikali ya Rais Samia.

“Rais Samia tangu alipoingia madarakani, alikuwa karibu na sekta ya habari na kutoa matumaini ya kufanyiwa marejeo kwa sheria hii ya mwaka 2016. Na tayari matokeo yake ni wadau wa habari na serikali kukaa kwa pamoja na kuainisha vipengele gani tungependa viondolewe,” alisema.

Amefafanua , kazi iliyobaki sasa ni upande wa serikali kukamilisha mchakato na kisha mapendekezo hayo kupelekwa bungeni kwa mujibu wa sheria za nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, alisema mchakato huu unakwenda kwa kuwa, Rais aliyepo madarakani ana dhamira njema na sekta ya habari.
Previous Post Next Post