IBADA YA MKESHA MKUBWA WA WANAVYUO KUFANYIKA KESHO KATIKA UWANJA WA UHURU (USIKU WA SIFA)


Na Mwandishi Wetu

Umoja wa vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali kutoka jimbo kuu la Dar es Salaam wameandaa tamasha kubwa lenye lengo la kuinjilisha kwa njia ya mkesha hasa katika kuwaombea vijana, kusali, kuabudu, kumtukuza na kumshukuru Mungu lakini pia kuliombea Taifa kwa ujumla.

Hayo aliyasema Padri wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kassembo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kuhusu mkesha huo ambao unatarajiwa kuanza leo ijumaa Desemba 16, 2022 na kumalizika kesho Jumamosi.

Aidha Padri Kassembo alisema lengo lingine la Mkesha huo ni kuwafanya vijana wawe na hofu ya Mungu katika kila jambo wanalolifanya.


"Vijana wanamambo mengi hivyo wanahitaji neema za Mungu,ndiyo maana wameamua kuwashirikisha na vijana wenzao kuja na tamasha hili ambalo litawafanya wawe na hofu ya Mungu "

Pia Padri Kassembo akiwakaribisha vijana wote katika jimbo lao kuu la Dar es salaam kuja kushiriki katika mkesha huo lakini pia wazazi wawaruhusu vijana waje katika mkesha huu waweze kusali, kuabudu, na kumtukuza Mungu kwa pamoja.





Kwa upande wake Mratibu Karesmatiki kutoka kanisa katoliki jimbo kuu dar es salaam, Ludovick Kawishe alisema Tukio mkesha huo utakua ni wa kipekee sana kwani vijana wanapokutana watajengeana uwezo, na kubadilisha mawazo ambapo watakua na hofu ya kuendelea kumtumikia Mungu lakini .

Pia alimshukuru baba askofu kwa kukubali kwenda kusali pamoja nao katika mkesha huo lakini pia vijana wa vyuo ambao wameweza kupata maono ya kimungu kuweza kuwakutanisha vijana wengine kwenda kumshukuru Mungu.

Naye Katibu Maandalizi ya mkesha wa usiku wa sifa, Ronaldo Chota alisema Mkesha huo hauna kiingilio na wamewalenga sana wanafunzi wa vyuo ambao baadhi yao hupenda kujihusisha na makundi yasiyofaa, ambapo tayari wamevifikia vyuo 51.

"Kumekua na baadhi ya tabia ambazo vijana wanajiingiza katika maadili yasiyofaa na kuiga tamaduni zisizo za kitanzania ambapo kupitia ibada ya misa na kumsifu Mungu watapata mafundisho ambayo yatawafanya kuwa na hofu ya Mungu na kupelekea kupata viongozi bora nchini"

Pia alisema kwa mwaka huu wanatarajia kuongeza idadi ya washiriki tofauti na ilivyo kwa mkesha uliopita.

"Mkesha wa mwisho tulikusanya vijana 15000 na mwaka huu tunatarajia kukusanya vijana takribani 30,000"
Previous Post Next Post