MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKEMEA VITENDO VYA UONEVU, UNYANYASAJI NA UKATILI KATIKA MAENEO YA KAZI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Hafla ya Utoaji Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikabidhi tuzo kwa Benki ya NMB ilioshinda kuwa Mwaajiri Bora wa Ujumla wa Mwaka 2022 wakati wa Hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam. (Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Jayne Nyimbo).


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa vipengele mbalimbali vya waajiri bora wa mwaka 2022 wakati wa Hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa vipengele mbalimbali vya waajiri bora wa mwaka 2022 wakati wa Hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.



Na Lilian Ekonga, Jijin Dar es salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amekemea vitendo vya uonevu, unyanyasaji na ukatili katika maeneo ya kazi ambayo husababisha wafanyakazi kudhalilishwa na kuwa wanyonge mahali pa kazi hususani manyanyaso ya umri, jinsia, rangi, kabila, ulemavu pamoja na dini.
 
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Hafla ya Utoaji Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam. Ambapo Amesema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na vinaathiri utendaji wa kazi sio tu kwa waathirika, bali kwa viongozi na Taasisi au Mashirika wanayofanyia kazi

Makamu wa Rais Ameongeza kuwa kila mfanyakazi ana haki ya kutendewa utu, kuthaminiwa na kuheshimika kazini na kuagiza kuwekwa mifumo itakayowezesha wafanyakazi kutoa taarifa za kunyanyaswa au kuonewa bila kuhofia madhara yoyote yanayoweza kujitokeza ikiwemo kupoteza ajira zao.
 
Halikadhalika Makamu wa Rais ameiagiza  Wizara ya Kazi kutoa elimu kwa waajiriwa kujua haki zao na pia kuhakiki aina ya mikataba inayotolewa ili ikidhi vigezo vyote muhimu ikiwa ni pamoja na kuainisha wajibu na haki za mwajiri/mwajiriwa kwenye masuala ya afya, likizo, ulemavu, mafao na migogoro.
 
Pia amewasisitiza waajiri kuzingatia sheria zilizopo kuhusu ajira kwa wageni ikiwemo kuhakikisha nafasi zisizo za kitaalamu au ambazo utalaamu wake unaweza kupatikana hapa nchini hazitolewi kwa wageni.

 Amesewasihi waajiri kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na tija yao katika uzalishaji ili waweze kujikimu kimaisha kulingana na wakati  ikiwa ni pamoja na kutoa posho, tuzo na motisha mbalimbali ili kutambua mchango mkubwa wa wafanyakazi bora katika taasisi, kuwapandisha vyeo na kuwapatia stahili zinazoendana na nafasi zao.
 
Makamu wa Rais amewataka kutumia tuzo hizo kuwa chachu ya kuboresha mazingira ya mahali pa kazi na kuhamasisha utendaji wenye tija kwa manufaa ya taasisi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. 

Aidha, amewahakikishia  kuwa kupitia Serikali, Vyama vya Waajiri na Vyama vya wafanyakazi kuendelea kujadiliana masuala mbalimbali  yanayohusu Ajira na Kazi nchini ili kuboresha na kutatua changamoto zilizopo kwa pamoja. 

" Serikali chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imejipanga kuhakikisha sheria na sera za nchi zinakidhi mahitaji ya waajiri na waajiriwa"Amesema 
 
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu  Prof. Joyce Ndalichako amesema  Serikali imekamilisha upangaji wa Kima cha Chini cha Mshahara katika sekta binafsi na kima hicho tayari kimeshatangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 687 la tarehe 25 Novemba, 2022. -  

"Nitumie fursa hii kuwafahamisha rasmi kwamba kima hicho mitaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 01/01/2023.  Ikumbukwe kwamba kwa miaka 9 iliyopita (toka mwaka 2013) kulikuwa hakuna tamko rasmi la Kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi" Amsema prof Ndalichako.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya ATE amesema wanafuraha kama Bodi kwa mwaka huu 2022 wamewwza kuziandaa na kuzitoa kwa kipindi cha miaka miwili hakuweza kufanya mchakato huu kutokana na janga la korona. 

Washindi we wa tuzo za mwajiri bora ni pamoja na Geita Gold Mine, SBL, TPA, NMB Bank, Coca-Cola, CRDB, Vodacom Plc, Puma Energy, Serengeti breweries.
Washindi wa nafasi ya tatu tuzo ilienda kwa Geita Gold Mine, nafasi ya pili Tanzania Breweries Limited na mshindi wa jumla alikuwa NMB Bank.
Previous Post Next Post