TANESCO YAELEZEA JITIHADA ZA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA UMEME


Na Lilian Ekonga

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa ya jitihada za muda mfupi na za mda wa kati zilizochukuliwa katika kukabiliana na upungufu wa Umeme ambapo mabwawa yote ya kufua umeme na matengenezo ya mitambo yaliyobakia kukamilika kama yalivyopangwa. 

Akizungumza na waandishi na waandishi wa Habari Leo Disemba 2 , Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, amesema hali ya umeme itaendelea kuimarika hivyo inatarajiwa kiasi cha upungufu wa umeme kwa siku kuendelea kupungua kutoka wastani wa kati ya megawati 300 hadi 350 wiki iliyopita hadi kufikia megawati 215 za umeme wiki hii.

"Tayari tumeshakamilisha matengezo ya matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha kidatu na umeshaanza kuzalisha megawati 50 za umeme katika Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 30 Novemba 2022"amesema Mkurugenzi Mtendaji.

Ameongeza kuwa sababu Ukame bado inaendelea kutokana na mabwa kukosa maji licha ya mvua kunyesha lakin katika bwana yao hawajaona maji ya kutosha ya kuwezesha uzalishaji wa Umeme.

"Mtiririko wa Maji unaoingia kwenye mabwawa ya kihansi na pangani kwenye bwawa la Kihansi mtiririko upo chini unauweza kuzalisha megawati 17 na uwezo w wa kuzalisha ni megawati 180. amesema 

Ameongeza kuwa “matengenezo ya mtambo mmoja katika kituo cha Kinyerezi namba II yameshakamilika na tayari umeshaanza kuzalisha megawati 215 za umeme kuanzia tarehe 24 Novemba 2022”

Kuhusu jitihada za muda mfupi zinazoendelea kufanyika Maharage amesema kuwa majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea, na kwa sasa mitambo hii inaingiza jumla ya megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa.

“Tunategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba 2022, mitambo hii itakuwa inazalisha jumla ya megawati 90 kama tulivyoeleza hapo awali” amesema 

Aidha amesema mitambo mingine miwili inatarajiwa kuanza kufanya kazi katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I kuanzia mwezi Februari 2023 ili kuingiza megawati 90 za umeme katika Gridi ya Taifa.
Previous Post Next Post