HALMASHAURI WILAYA YA KARAGWE YAISHUKURU SERIKALI YA AWAMU YA SITA KWA KUIPA FEDHA ZA UJENZI WA MIRADI MBALIMBALI


Na Mwandishi Wetu, Karagwe 

Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera inampongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha  nyingi kwenye halmashauri hiyo kwa ajili ujenzi  wa vyumba vya madarasa katika baadhi ya shule za Sekondari zilizopo wilayani humo pamoja na ukamilishaji wa majengo katika hospitali ya wilaya ya karagwe.

Moja ya fedha hizo  shilingi Bilioni 1.32 zimeelekezwa kwenye utekeleza wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 66 kwa mwaka huu wa fedha ndani ya wilaya ya karagwe ambapo lengo kuu ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajia kuanza mwaka  2023.


Hayo yameelezwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Michael Nzyungu wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Desemba 7 mwaka huu ambapo amesema kuwa  shule moja wapo iliyopewa fedha ni shule ya Sekondari Rugu iliyopo   kitongoji cha Nyakahanga kijiji cha Rugu wilayani humo kwaajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.

Amesema kuwa madarasa yote 66 yapo kwenye hatua tofautitofauti za kuezeka na umaliziaji  na hatimaye  baada ya muda mfupi madarasa yote yatakuwa yamekamilika, kwa Halmashauri nzima.
Nzyungu amesema kwaniaba ya wananchi wa karagwe  anamshukuru sana Rais Dk.Samia Suluhu Hassan  kwa kuwapa  fedha nyingi kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.


Pia Mkurugenzi huyo wa Halmashauri amesema kuwa kwa upande wa sekta ya afya Hospitali ya Wilaya ni kubwa ina majengo mengi makubwa na ya kisasa jambo ambalo Halmashauri hiyo inajivunia mradi huo mkubwa na wa kimkakati.

“Tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha hizo na kwamba fedha hizo zimeletwa kwa awamu nne awamu ya kwanza Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 kwa yale majengo waliyoelekezwa Halmashauri iliongeza kiasi cha shilingi milioni 300.”amesema 

 “Kwa hiyo awamu ya kwanza  ina majengo saba Jengo la Utawala, OPD, Maabara, Exray, Wodi ya wazazi pamoja na mambo mengine ambayo yalitumia kiasi cha shilingi Bilion 1.8, na Bilioni1.5 zilikuwa za serikali kuu na Halmashauri ikatoa Milioni 300, hiyo ilikuwa ni awamu ya kwanza 2001,” amesema Nzyungu.


Mwaka 2002 walipata awamu ya pili walipata shilingi milioni 500 kwaajili ya kujenga wodi tatu na zimekamilika  kuna wodi ya wanaume, wodi ya wanawake na wodi ya Watoto kwamba kwa fedha hizo hazikukamilika Halmashauri ilichangia kwa kuongeza shilingi milioni 60 na kwa sasa ujenzi wa mashimo ya maji taka unaendelea.

Ameongeza kuwa awamu ya tatu ni fedha za uviko kiasi cha shilingi Milioni 340  ambapo shilingi Milioni 90 ilitumika kujenga nyumba ya mtumishi inayofaa kuishi familia mbili tofauti na Milioni 250 ilitumika kujenga jingo la wagonjwa Mahututi (ICU) na tayari limeanza kutumika na kama Halmashauri umaliziaji wameongeza shilingi Milioni 40.

Amesema kuwa kwa awamu ya nne inayoendelea ni fedha walizopata kipindi cha mwaka jana shilingi milioni 800 mwishoni mwa mwaka huu wa fedha kwaajili ya kujenga wodi za wanawake, wanaume na chumba cha upasuaji pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari) na kufafanua kuwa kuna majengo yamekamilika kama Mochwari lakini na majengo mengine yanaendelea kukamilika.

“Nachoshukuru Serikali ya awamu ya sita imetupendelea sisi Karagwe tuna majengo mengi sana na tunaendelea kupokea vifaa lakini changamoto kubwa uhaba wa watumishi hawatoshi unajua Karagwe ni mbali na tukipata watumishi hawaji wote, changamoto nyingine ni ukosefu wa Ambulance zilizopo ni mbili moja linatumika Wilayani na lingine kwenye vituo vya afya vijijini,” amesema Mkurugenzi.

Pia mkurugenzi ameongeza kuwa moja ya miradi wanayotekeleza kwa fedha za ndani ni ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ambapo wameingia makubaliano mwekezaji wa ndani na kwamba itakapo kamilika mwekezaji huyo ataimiliki kwa muda wa miaka saba na baada ya hapo itarudi mikononi mwa Halmashauri kwa asilimia 100.
Mwisho.
Previous Post Next Post