CHUO CHA NIT CHA PONGEZWA KWA MAGEUZI YA KUPANUA WIGO WA MITAALA


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam. 

Mkurugenzi wa uthibiti wa Barabara, Eng Johansen Kahatano amekipongeza Chuo cha taifa cha Usafirishaji(NIT) kwa mageuzi ambayo wameyafanya kwa kupanua wigo wa mitaala na kufikia maeneo mengi ya usafirishaji ikiwemo, barabara, reli , anga, maji na bomba 

Ameyasema hayo leo Disemba 8 katika kongamano la 9 la kuwapongeza wahitimu wa chuo cha NIT waliofanya vizuri katika masomo ya nadharia na vitendo katika chuo cha Taifa cha usafirishaji.

"Wameongeza wahitimu wengi na tumeshuhudia wahitimu wakifanya vizuri katika maonyesho ambavyo wamekuwa wakifanya kwemye makongamano."amesema Eng Kahatano. 


Hata hivyo amesema kwa kuwatia moyo wanafunzi wanao hitimu wameamua kutoa zawadi ya shilingi milion 1 na kwa wanafunzi wa bora aliye fanya vizuri na nafasi ya mazoezi kwa wanafunzi watano ambao wamefanya vizuri ili kuwajengea uwezo na kuwatia moyo ili wengine waweze kufanya vizuri. 

Aidha amesema kutokana na swaka la ajali za barabarani wahitimu hao wanaweza kusaidia kupunguza kwa kuzingatia kile walichofundishwa na kuunda mitambo bora ya kupunguza ajili hizo.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha usafiri, Dkt Prosper Mgaya amesema kongamano hilo linawaunganisha wanafunzi waliomaliza mwaka huu na kwenda kuwaunganisha ma wenzeo ambao walishamaliza NIT na kuingia kwenye umoja ambao wa wanafunzi waliomaliza chuo cha taifa cha usafirishaji.

Amesema kuwa mwaka huu chuo cha NIT kimejikita kwenye usafiri wa reli kwa sababu serikali inawekeza fedha katika usafiri wa reli.

"Chuo kipo tayar kuanzisha kitengo cha mafunzo ya usafiri wa reli ambapo kituo kitakuwa mkoani Tabora na kituo hicho kimethaminiwa na serikali ya awamu ya sita."amesema.

Pia amesema kwa upande wa usafiri wa Anga wanategemea ndege mbili za mafunzo ya urubani kukabithiwa na serikali hivi karibuni. 

"Serikali inawekeza katika ununuzi wa baadhi ya miundombiunu ikiwemo meli, mabehewa na ndega sisi kama chuo cha usafirishaji tunakazi kubwa ya kuzalisha watumushi ambao watasaidia kuendesha hiyo miundombinu."amesema Dkt Prosper
Previous Post Next Post