Na Lilian Ekonga Dar es salaaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba anatarijiwa kuwa mgeni Rasmi katika Mahafali 15 ya chuo cha kodi (ITA) ambapo atatunuku vyeti vya stashahada, Shahada na stashahada ya Uzamili kwa wahitimu 489 kutoka chuo hapo
Hayo yamesemwa Leo November 23 na Mkuu wa Chuo Cha Kodi, Prof Isaya Jairo wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema Mahafali hayo yatanyika tarehe 25 novemba 2022 jijini Dar es salaam katika ukumbi uliopo chuoni hapo kuanzia saa tatu Hasubuhi.
"Kuna ongezeko la asimilia 25.1 ya ya wahitimu kwa mwaka huu 2022 ukilinganisha na wahitimu 387 ambapo walihitimu mwaka 2021, ongezeko hili linatokana na jitihada za chuo kuhakikisha viwango vya mafunzo yanayotolewa na chuo vinakidhi matakwa ya mahitaji ya taaluma na kodi" amesema Prof Isaya.
Ameongeza kwa kuzingatia mahusiano na ushirikiano uliopo kati ya Chuo na Mamlaka za Mapato za Afrika chuo kimewaalika baadhi ya wakuu wa Mamlaka za Mapato mbalimbali ambapo tayari baadhi wamethibitisha Kushiriki.
Aidha amesema Chuo cha kodi kinatoa mafunzo yanayoendana na mabadiliko ya sayansi, teknolojia na uchumi yanayolenga mahitaji ya soko la wataalamu katika nyanja za forodha na kodi hapa nchini na barani Afrika.
"Nachukua Fursa Hii kuwakaribisha, wageni waalikwa wote , wahitimu pamoja na wazazi katika Mahafali haya ya 15 ya chuo cha Kodi," Amesema.