PWC na Techno Auditors kuvaana fainali ya NBAA, Novemba 28


Na Humphrey Msechu 

FAINALI ya kukata na shoka kati ya PWC dhidi ya Techno Auditors "afe beki afe kipa lazima kieleweke" mashindano hayo ya mpira wa miguu ya maadhimisho ya 50 ya NBAA inatarajiwa kucheza mnamo Novemba 28, 2022 saa 10 jioni katika uwanja wa TPDC jijini Dar es Salaam.


Timu ya PWC Tanzania ilikuwa ya kwanza kutangulia hatua ya fainali ya mashindano hayo baada ya kuindosha timu ya KPMG kwa mabao 2-1, mchezo ambao ulikuwa wa aina yake kwa kuwakutanisha miamba hao wa soka.

Techno Auditors wamefanikiwa kuwatupa nje ya michuano hiyo timu ya PKF kwa kuichapa kichapo cha mabao 2-1 na kutandaza soka safi, na kudhamiria kuwa wanataka kombe hilo kwa kila hali na kutuma salamu kwa timu ya PWC Tanzania wajiandae vizuri.


Hivyo, ikumbukwe michuano hiyo ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania NBAA ambayo wameandaa mashindano hayo kama shamrashamra katika kuadhimisha miaka hiyo.
Previous Post Next Post