WAZIRI NAPE: HAKUTAKUWA NA MABADILIKO YA BEI ZA BANDO


Na Lilian Ekonga. 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hakutakuwa na mabadiliko ya bei za bando yoyote hadi tathmini ya gharama itakapokamilika. 

 Ameyasema hayo leo Novemba 21, 2022 wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema tathimini hiyo inayofanywa kila baada ya miaka mitano, inatarajiwa kukamilika kati ya Desemba 2022 hadi Januari 2023.

Nape amesema kwa sasa watoa huduma wote wako katika viwango vya bei elekezi iliyowekwa na Serikali ambayo ni kati ya Sh2.03 hadi Sh9.35.


"Hatutegemei mabadiliko yoyote kwa kipindi hiki hadi tathmini itakapokamilika, niwaombe wananchi wasione hatuhangaiki na suala hili, tumekuwa tukihangaika nalo. amesema nape

Ameongeza kuwa kwa Sasa wamefikia hatua ambayo watatulia hadi tathmini itakapokamilika na matumaini yao kuwa itawapa muelekeo mzuri. 

Aidha Waziri amesema kuwa serikali ya Awamu ya sita ni kuhakikisha taasisi zake zinafanya kazi kwa ufanisi na kuwahudumia watanzania kwa mujibu wa sheria , kanuni na maelekezo yanayotolewa kupitia maelekezo ya kisera
Previous Post Next Post