WAGANGA WA JADI WASHAURIWA KUACHA KUWARUBUNI WANANCHI WANAOSUMBULIWA NA UGOJWA WA MATENDE NA MABUSHA


Na Lilian Ekonga, jijin Dar es salaaam

Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amewashauri waganga wa jadi pamoja na tiba asilia kuacha kuwarubuni wananchi wanaosumbuliwa na ugonjwa wa matende na mabusha ili wakapate tiba sahihi dhidi ya ugonjwa huo ambayo hutolewa na serikali.

Dkt Rashid ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi utoaji dawakinga dhidi ya ugonjwa wa matende na mabusha katika kata ya Tandale jijini Dar es Salaam ikiwa ni miongoni mwa kata zinazoongoza kuwa na wagonjwa wa matende na mabusha kwa asilimia 3 katika jiji hilo.


"Dawa ambazo hazina madhara yoyote na dawa salama na zinatukinga dhidi ya ugojwa wa matende na mabusha, Msiwe na hofu kwamba hizi dawa zinapunguza kitu mwili hakuna"amesema Mfaume. 

Kwa upande wake katibu tawala manispaa ya Kinondoni Stellah Msofe akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi huo amewaasa wananchi kutonasibisha dawakinga hizo na imani potofu kwani athari za ugonjwa huo ni kubwa na hugharimu serikali fedha nyingi.


Amesema kuwa katika Kata ya tandale hali ya ugojwa wa matende na mabusha imekuwa ipo juu sana ukiacha na kata zote za mkoa wa dar es salaam ambapo kuna asilimia 3.82 ya wagojwa ikifuatiwa na kata ya bunju ambapo wapo kwenye asilimia 2.

"Dawa zinatolewa hapa hazina madhara yoyote na niwaombr wananchi waepuka maneno ya uwongo yanayopakizwa kwao kuhusu dawa hizi"amesema Msofe


Pia Stellla amewasihi wananchi wajitokeze kwa wingi na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu afya ili waweze kutapatiwa dawa hizo. 

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamekiri kuwa baadhi yao wamekuwa wakinasibisha ugonjwa wa matende na mabusha na imani za kishirikina huku wakiiomba zoezi la utoaji elimu ya ugonjwa huo kuwa endelevu.
Previous Post Next Post