WABUNGE WAPITISHWA KWENYE BAADHI YA VIPENGELE VYA SHERIA YA HABARI YA MWAKA 2016


Na Humphrey Msechu

Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania(MISA TAN), James Marenga pamoja na Mwenyekiti na Jukwaa la Wahiriri Tanazania (TEF) Deodatus Balile, wamewapitisha wabunge kwenye baadhi ya vipengelea vya sheria ya habari ya mwaka 2016 na mapendekezo ya wadau wa habari.

Hayo yamefanyika jijini dodoma tarehe 10 November 2022 katika kikao cha mazungumzo na baadhi ya wabunge , kwa lengo la kuongeza ufahamu kuhusu mabadiliko ya sheria ya habari.


Pia wabunge hao waliweza kupata nafasi ya kuuliza maswali ambayo baadaye yalitolewa ufafanuzi kutoka kwa balile na Marenga.


Pamoja na hayo aidha wabunge hao walielezea kufurahishwanna umoja wa wadaunwa habari ulioundwa kwa ajili ya kusukuma mbele mapendekezo ya mabadiliko ua sheria ya habari.


Baada ya kukabithiwa kwa nakala za mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya habari, waliahidi kuendelea kufanyia kazi na hatimaye kuwa na uelewa wa juu ili jambo hilo litakapofikishwa mbele yao, wapate kuishauri serikali kwa malengo mapana ya taifa.
Previous Post Next Post