TEF KUHAKIKISHA TASNIA YA HABARI INAPATA SHERIA RAFIKI


Na Humphrey Msechu

Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania(TEF), ameongoza kikao kilichojumuisha wadau wa Haki ya kupata Habari(CoRi) na uongozi wa TEF katika kuhahakisha tasnia ya habari inapata sheria rafiki.

Kikao hicho kilichofanyika jijin dodoma, tarehe 8 Novemba kilihudhuriwa na Mbuge wa Ukonga (CCM), Dar es salaam, Jerry Silaa ambapo amehaidi kushirikiana na wabunge wenzake katika kuhakikisha tasnia ya habari inakuwa na sheria nzuri.

"Mimi na wabunge wenzangu tutashirikiana. Dunia imebadilika na hatuwezi kubaki hapa tulipo" amesema 

Jerry silaa ameongeza kuwa atazungumza na wabunge wenzake kisha wataona namna ya kufanya kuhusiana na sheria ya habari.

Nae mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile alimweleza jerry kwamba, sheria ya habari ya mwaka 2016 imeweka mazingira makubwa ya kumuhofisha mwandishi wa habari. 

Na kwamba, ndani ya sheria hiyo kuna vipengele mbalimbali kwa undani wake, vinaua tasnia ya habari akitolea mfano kipengele kinachompa nguvu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kufungia chombo cha habari kwa namna anavyoona inafaa.

‘‘Katika safari ya mabadiliko haya, tumeungana taasisi zote za habari ili kuwa na kauli moja. Tumeunganisha nguvu ili kufikia lengo ’

James Marenga, Mjumbe wa CoRI kutoka Taasisi ya Vyombo ya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania alimweleza Jerry kwamba, tasnia ya habari haina tofauti na tasnia nyingine nchini katika utendaji kazi.

Marenga amabaye ni wakili wa kujitegemea amesema ikiwa mawakili wanatengeneza taratibu zao na kuzifanya kuwa rejea katika kazi zao, inashindikanaje wanahabari nao wakajiwekea utaratibu wa ‘kujihukumu’ kama ilivyo tasnia nyingine? 

‘‘Mimi ni mwanasheria, katika taasisi yetu tulitengeneza cord of conduct wenyewe na hizo ndio zinatuongozi, ni busara na wanahabari wakawa na utaratibu wao kisheria unaosimamiwa na wenyewe katika kuhakikisha maadili ya uandishi wa habari yanafuatwa,’’ amesema.

Jessy Kwayu, Mkurugenzi Mkuu wa Media Brains Inc Ltd alisema, sheria ya habari ya mwaka 2016 ilipitishwa katia mazingira ambayo si rafiki.

‘‘Vipengele 19 vya sheria hiyo vilijaribiwa kwenye sheria za nchi, vikaonekana kutoingia katika mizani ya kisheria,’’ amesemab Kwayu.

Rose Reuben, Mkurugenzi Mkuu wa alisema, kwa mazingira ya sasa, waandishi wanashindwa kuandika habari kwa uhuru.
Previous Post Next Post