BALILE: SERIKALI YATAKIWA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA VIFAA VYA UOKOAJI


Na Humphrey Msechu

Serikali imetakiwa kufanya uwekezaji mkubwa katika mafunzo na vifaa vya uokoaji ikiwemo helikopta katika matukio ya ajali kufuatia ajali ya ndege ya Precision iliyotokea hivi karibuni Mkoani Kagera.


Wito umetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile wakati wakitoa taarifa ya kupokea kwa masikitiko vifo vya watu 19 kutokana ajali ya ndege iliyotokea novemba 6, 2022.


Aidha TEF imesema inatambua na kupongeza juhudi za uokoaji zilizofanywa na wavuvi wadogo katika ajali ya Precision iliyotokea Mkoani Kagera. 

Katika hatua nyingine jukwaa hilo limetoa mapendekezo wavuvi waandaliwe kama jeshi la akiba la uokozi kama ilivyo kwa mgambo kwenye Jeshi la Nchi Kavu.
Previous Post Next Post