TCRA yawafungulia milango wabunifu TEHAMA


Na Humphrey Msechu 

MKURUGENZI mkuu wa TCRA, Dkt. Jabir Bakari amesema Serikali ya Tanzania imewafungulia milango muhimu vijana wabunifu katika Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuwapa uwezeshaji uliokuwa unakwamisha ubunifu miaka mingi.

Dkt. Bakari amesema TCRA kwa ushirikiano na taasisi nyingine imeweka mazingira rafiki kwa vijana wabunifu wa TEHAMA kutengeneza fursa za kukuza ubunifu na hatimaye kuzaa ajira kwa vijana  nakutakiwa kubwa na vifaa vya gharama nafuu vya TEHAMA kama vile kompyuta mpakato na simu ya kiganjani au vifaa rununu pendwa kama vile kishikwambi kukamilisha ubunifu wake.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Jabir, amesisitiza kuwa vijana wabunifu na wavumbuzi wa programu mbalimbali za kidijitali sasa wanaweza kujitokeza kupata rasilimali hizo zitakazowawezesha kupata fursa ya kutengeneza ajira; kujiletea kipato na kutatua changamoto mtambuka za jamii.

“Tumejipanga kuhakikisha wabunifu wapya hasa wa sekta ya TEHAMA wanaoweza kutatua changamoto za jamii yetu wanapata rasilimali hizi za mawasiliano, ili washiriki katika uchumi wa kidijiti,” amesisitiza Mkurugenzi Mkuu Dk. Jabir.

Wameweka utaratibu jinsi ya kusaidia vijana hawa: “Tuna utaratibu wa kutoa rasilimali hizi kwa muda wa miezi mitatu; ambazo tunatoa [kwa mbunifu] baada ya kuidhinishwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia ambayo hujiridhisha kubaini kama wazo la kibunifu linakidhi kufanyiwa majaribio na hapo ndipo tunatoa rasilimali za masafa au misimbo ya namba fupi kwa muda wa majaribio wa miezi mitatu,” amebainisha Dk. Jabir

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, ina jukumu la kukuza ubunifu katika TEHAMA kwa nia ya kukuza uchumi za kidigiti. Sekta ya mawasiliano ni sekta-wezeshi ya sekta nyingine muhimu kwenye uchumi wa nchi kama vile, usafirishaji, nishati, afya, elimu, viwanda, kilimo na huduma mbalimbali kama huduma za kifedha. 

Moja ya Malengo ya Kimkakati ya TCRA ni Kukuza Ubunifu, uzalishaji wa maudhui ya ndani na ujanibishaji (localization). 

Katika kulitambua hilo, TCRA huratibu vikao vya mashauriano na wadau wakuu wanaojishughulisha na ubunifu kujadili masuala yanayohusu fursa na changamoto za programu za ubunifu wa TEHAMA kukua na jinsi TCRA inavyoweza kuweka mazingira wezeshi; ikizingatiwa kwamba Mamlaka hiyo ni taasisi wezeshi katika sekta pana ya Mawasiliano.

Utoaji wa Rasilimali za Mawasiliano Ili kukuza ubunifu na utafiti katika TEHAMA, unabainisha kuwa TCRA imedhamiria kuweka mazingira wezeshi kwa wabunifu wanaotaka kutumia rasilimali za mawasiliano kufanya majaribio ya mawazo mbalimbali ya ubunifu/utafiti.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeondoa malipo ya ada ya maombi na usajili wa leseni wa rasilimali hizo kwa ajili ya wabunifu wenye nia ya kubuni suala lolote litakalorahisisha mazingira ya kawaida ya kila siku ya mwananchi.

Wabunifu wanaotaka kutumia fursa hii wanaweza kuwasiliana na Dawati la Huduma la TCRA kupitia namba 0800008272 au kutembelea tovuti www.tcra.go.tz

Previous Post Next Post