Dkt. Gwajima: Serikali kuimarisha mifumo kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwa wajane


Na Humphrey Msechu

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wajane kuchangamkia fursa za kiuchumi kwa kujiunga katika vikundi na taasisi za kuwawezesha kiuchumi, kuepuka, umaskini na utegemezi katika jamii.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chama cha Wajane jijini Dar es salaam Waziri Gwajima amesema Serikali haitafumbia macho yeyote anayemnyanyasa mjane au kumdhulumu haki yake, hivyo kwa wale wanaofanya amewataka kuacha mara moja.


"Msiogope kujiunga katika vikundi na taasisi za kuwawezesha kiuchumi, kuna majukwaa ya kuwawezesha wananchi kiuchumi" amesema Waziri Gwajima


Aidha, Waziri Dkt. Gwajima ametoa wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kuandika wosia ili kuepusha migogoro ndani ya familia kwa sababu inaathiri wajane na watoto.

Hivyo, Dkt. Gwajima amesema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwa wajane.
Previous Post Next Post