PROF MKENDA : SOMO LA KIARABU LIFUNDISHWE KIDATO CHA TANO NA SITA


Na lilian Ekonga jijini Dar es salaam

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema atalipa msukumo somo lenye kombinesheni kiarabu ili lifundishwe kidato cha tano na cha sita kwa sababu itasaidia kuzalisha wataalam wataokwenda kukalimani kiarabu na kiswahili kwa kuwa ni lugha kubwa inayotumika umoja wa mataifa.

Profea Mkenda ameyasema hayo katika Mahafali ya kidato cha nne iliyojumuisha shule za kiislamu 11 jijini Dar es salaam.ambapo amesisitiz kuhusu somo la dini bado lipo kwenye mjadala ikiwamo masuala muhimu ya kuzingatia.

Aidha ametoa wito kwa wamiliki wa shule binafsi na shule za umma kusimamia maadili na malezi kwani serikali haitomfumbia macho yeyote atakaekiuka miiko na maadili iliyowekwa.


"Serikali inalaani vikali walioruhusu vitendo katika shule ya pwani na inaendelea kufuatilia sakata hilo na itachukua hatua kali kwa kila mwalimu aliyehusika na tukio hilo kwa sababu sio rahisi wanafunzi kufanya vitendo hivyo bila mwalimu yotote kuwa na taarifa,"amesema prof Mkenda.

Waziri Ameongeza kuwa Serikali inazihitaji shule binafsi kwa sababu zimesaidia wazazi kutopeleka watoto nje ya nchi na kuwatafutia fursa za kielimu hali iliyochangia kufuatilia malezi na makuzi yao.

Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Dk. Musa Salim, amesema katika uislamu suala la elimu limepewa kipaumbele, kwamba tangu mtu anapozaliwa hadi anapofariki anapaswa kuendelea kujifunza hivyo kuwataka wanafunzi hao kuishika elimu.


"Tunawahusia watoto wetu, tunaowaaga leo na watakaoendelea,kushikamana na maadili, elimu haina maana yote mbele ya jamii iliyokosa maadili, .nyinyi ndio taifa la baadaye, nchi hii inawategemea katika suala la madili, endapo taifa litakosa maadili ni sawa na kusema taifa hilo ni mfu" amesema 

Pia ameitaka jamii ya kiislamu kujitafakari kwa kuwa ndio inayoongoza kwa mmomonyoko wa maadili, huku kati ya panya road 10, saba ni waislamu,jambo linaloitia aibu serikali na jamii kwa ujumla.

Nae Mkuu wa Shule ya Al Haramain, Buhero Issa, amesema kuwa mahafali hayo yanafanyika kwa mara ya 11 na kuhusisha shule 11 za kiislamu kutoka Dar es Salaam ikiwamo shule za sekondari Kunduchi na Ununio, Tekeme Islamic, Muzdarfa Islamic, Dar es Salaam Islamic, Al Haramain na Hijra Islamic, Nuru Islamic na Kinondoni Muslim, 

Ameongeza kuwa shule hizo zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma na mwaka jana asilimia 98 ya wanafunzi katika shule hizo walifanikiwa kujiunga na kidato cha tano. 

 "Shule hizo zinapitiwa na changamoto ya mmomonyoko maadili ya wanafunzi, na kumshukuru waziri wa elimu kwa kupitisha waraka wa kiistoria wa kimaadili, na kuweka vipindi mbalimbali vya dini ili kuwajenga wanafunzi" amesema

Pia amesema Somo la dini linakosa mvuto na wanafunzi kutolipa umuhimu kwa sababu limefanywa kuwa la hiyari,kukosa walimu husika, kutohisabiwa katika madaraja kidato cha nne, mitihani ya dini latika elimu ya msinga kutotahiniwa na Baraza la Mitihani (NECTA).
Previous Post Next Post