TAMASHA LA KUSAIDIA WATOTO WENYE ULEMAVU KUFANYIKA KATIKA PORI LA AKIBA PANDE

  
Na Mwandishi Wetu,
Dar es salaam.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wananyapori  nchini (TAWA) kupitia Pori lake la Akiba la Pande kwa kushirikiana na Dar running Club na Taasisi ya Africa Foundation for inclusive Communities (AFIC) wameandaa tamasha la mbio za hisani zenye lengo la kuwasaidia watoto wenye ulemavu wanaoishi mitaa inayozunguka pori hilo.

Ambapo tamasha hilo linalofahamika kama 'Pande Trail Running & Cycling' linatarajiwa kufanyika tarehe 19 Novemba mwaka huu huku likitarajiwa kujumuisha michezo mbalimbali ikiwemo kuendesha baiskel na kukimbia.
 
Afisa Mahusiano Mkuu wa TAWA, Vicky Kamata, amesema tayari taratibu zote zinaendelea za maandalizi ambapo tamasha hilo litawezesha walemavu hao kupata vifaa vya mazoezi.

"Sote kwa pamoja tuendelee kujisajili ilikuweza kushiriki Tamasha hili la Pande Trail Running & Cycling'.


Ambapo kupitia kwa kila mshiriki atapata nafasi ya kuchangia gharama za kununua vifaa hivyo" alieleza Mhe.Kamata wakati kikao cha maandalizi katika ofisi za Pande ukiwakutanisha Mkuu wa kituo cha Pande, Honest Bureta, Mustafa Buyogela afisa utalii kutoka Pande, Erasto Mtweve na Joseph Katembo kutoka Dar Running Club pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa AFIC Tanzania, Bw.Michael Mihayo.
 
Watoto hao wenye ulemavu wanasimamiwa na Taasisi ya Africa Foundation for Inclusive Communities (AFIC) ambapo katika Tamasha hilo pia kutakuwa na mambo mengine mengi kwa washiriki.

Previous Post Next Post