WAAJIRI NCHINI WAMETAKIWA KUWEKA MIFUMO YA KUWAWEZESHA WAFANYAKAZI KUFANYA MAZOEZI


Na Lilian Ekonga Dar es salaaam

Waajiri nchini wametakiwa kutenga siku maalumu kwa ajili ya wafanyakzi wao kufanya mazoezi ili kuweza kujikiinga na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam , na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako katika kilele cha Waajiri Health Bonanza ambapo Amewapongeza ATE kwa kuandaa bonaza hilo lenye malengo ya kuhamasisha na kuelimisha umuhimu wa usalama na afya mahali pa kazi kwa ustawi wa biashara.


Hata hivyo waziri ndalichako amesema kuwa waajiri nchini waweke mifumo ya kuwawezesha wafanyakazi kufanya mazoezi wakiwa kazini ikwemo kutenga sehemu ya maalumu ya mazoezi (GYM) ili kabla ya kufanya kazi mazoezi yaanze ili kupunguza magonjwa ya kuambukiza

Aidha Prof Ndalichako amesema magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yamekuwa yakiigharimu serikali hivyo angenda ya kutokomeza magonjwa hayo inafaa kuwa ya kila mmoja nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE), Suzanne Ndomba Doran, amesema kuwa waajiri wanatakiwa kuendelea kuweka mazingira ambayo ni salama kwa ajili ya kuangalia afya za wafanyakazi.


Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi TUCTA, Heri Mkunda amesema kuwa suala la mazoezi iwe ni tabia ya kila mfanyakazi.
Previous Post Next Post