Na Lilian Ekonga , Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana amezindua bodi ya makumbusho ya Taifa, itakayo saidia kuongeza ufanisj shughuli mbalimbali za Taasisi kufanyika Kwa haraka, vizuri na umakini.
Akizungumza katika Halfa Uzinduzi Huo uliofanya Leo Oktoba 22 jijini Dar es salaam, Waziri amesema bodi inajukumu la kuendelea kuongeza idadi ya watalii na kuongeza mikakati ya masoko mapya, tamaduni na Mila zetu tunazotakiwa kizihifadhi na maeno ya vivutio.
Pamoja na Uzinduzi Huo Waziri Chana amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuzindua Programu ya Tanzania Roral tour Ambayo imefungua milango Kwa watalii wengi Kuja Nchini.
"Watalii ambao wamekuwa wakija kwenye Makumbusho ya Taifa wameongeza kutoka Elfu sabuni mpaka kufikia laki Saba na Kuna Lengo kuendelea kuongeza Takwimu za watalii Nchini"Amesema Waziri Chana
Aidha Amesema Taasisi ya Makumbusho ya Taifa ni kati ya tasisi Muhimu ambapo imeweza kuongeza idadi Ajira za Moja Kwa moja na zisizokuwa za Moja Kwa moja takribani Million Moja na Laki tano (1500000).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho Oswald Masebo, Amesema msingi wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa ni kusimamia utendaji wa manejimenti ya shirika Katika kuhifadhi na kuendeleza uridhi wa utamaduni na kihostoria wa Taifa la kitanzania.
"Uridhi huu ndio unaolitambulisha Taifa la Tanzania na urithi huu ndio ambao unaleta taswira la ujenzi wa Taifa la Tanzania.Ndani ya urithi wa utamaduni na kihostoria Kuna fursa kubwa ya kiuchumi .
Masebo ameongeza kuwa Kazi ya bodi ni kuchochea hamasa ndani Makumbusho ya Taifa Ili kuchangia kufungua fursa kubwa za kiuchumi zilizopi kwenye fursa ya kiutamaduni na urithi wa kihostoria.
Nae Mkurugenzi wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Noel Lwoga Amesema kwakuwepo Kwa bodi yale ambayo Makumbusho imetengeza bila bodi yatakwenda kuimarika Zaidi Ili tuweze kufikia malengo Ambayo Serikali, Wizara na bodi imejiwekea Katika kufanikisha.
"Kama Makumbusho ya Taifa hapo kabla tulikuwa tukipata wageni si Zaid ya laki Saba tangu mwaka 1980 taasisi ilivyoanzishwa Ila hatuja vuka kiwango Cha k Cha Elfu sabini, lakin mwaka 2021, 2022 tumeweza kurekodi wageni laki Saba(700000) Kwa Asilimia 70 ni wageni wa ndani"Amesema