Wahariri wajengewa uwezo juu ya Mabadiliko ya sheria ya habari nchini


Na Humphrey Msechu

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limefanya warsha Kwa wahariri wa vyombo vya Habari yenye Lengo kuwajengea uwezo Waharirih Juu ya mipango ya uchechemuzi wa mabadiliko ya Sheria za habari.

Akizungumza Katika warsha hiyo, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile Amesema watakuwa mstari wa mbele kupigania mbadiliko ya Sheria zinazogusa tasnia ya habari Kwa kushirikiana na wadau wengine.

Hata hivyo Balile Amesema watahakikisha kunakuwa na sehemu ya kutatua matatizo yetu na yanayokabilu Jamii.

"Hatuwezi kukata marekebisho ya Sheria pasi na kushirikiana na Serikali Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali"Amesema Balile.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati tendaji ya Jukwaa la Wahariri, Salim Said Salim Amesema Waandishi wahabari wanatakiwa kusoma Sheria zinazogusa masuala ya habari na nyingine Ili wanapotaka zirekebishwe wawe na ushawishi mkubwa wa watunga Sheria.

"Bado Waandishi hatujawa na uelewa Mpana wa sheria zinazotuhusu, tufanye jitihada kuzijua. Tuwashawishi wenzetu Juu ya sheria zinazokwaza ukuaji wa tasnia ya habari na Maendeleo ya Taifa" Amesema 

Kwa uapnde wake , Sylvester Hanga amesema waandishi wa habari wanataka sheria za masuala ya habari ziwe rafiki ili zichochee demokrasia, haki za binadamu na maendeleo kwa Taifa.

Siylvester amesema Waandishi wa habari ni lazima wawe mstari wa mbele kuisemea jamii lakini ni lazima wahakikishe sheria zinazominya uhuru wa habari zinafanyiwa marekebisho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Naye mwezeshaji Tumaini Mbibo, amesema ni muhimu kwa waandishi wa habari kujua kiini cha matatizo yanayolikabili Taifa na njia za kutumia ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo husika.

 "Haki za binadamu zinakwenda sambamba na demokrasia hivyo uwepo wa sheria zinazominya tasnia ya habari zinakwamisha maendeleo hivyo vema ikafanyika mipango ya kufanya ushawishi wa mabadiliko" amesema.
Previous Post Next Post