Waandishi wa Habari wameaswa kujua haki na sheria zinazoongoza tasnia ya habari


Na Humphrey Msechu

Waandishi wa Habari wameaswa kujua haki na sheria zinazoongoza tasnia ya habari Ili atakapo kutana na makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo wabunge na kuwashawishi juu ya sheria zinazominya Uhuru wa habari na Haki za binadamu.

Rai hiyo imetolewa oktoba 21, na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim Said Salim wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo Wahariri juu ya mipango ya  mbadiliko ya sheria ya habari.

Amesema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kusoma sheria zinazohusu masuala ya habari na nyingine Ili wanapotaka zirekebishwe wawe na ushawishi mkubwa Kwa watunga sheria na jamii.

Bado waandishi hatujawa na uelewa mpana wa sheria zinazotuhusu, tufanye jitihada kuzijua. Tuwashawishi wenzetu juu ya sheria zinazokwaza ukuaji wa tasnia ya habari na maendeleo ya Taifa” amesema salim

Kwa upande wake , Sylvester Hanga amesema waandishi wa habari wanataka sheria za masuala ya habari ziwe rafiki ili zichochee demokrasia, haki za binadamu na maendeleo kwa Taifa.

Siylvester amesema Waandishi wa habari ni lazima wawe mstari wa mbele kuisemea jamii lakini ni lazima wahakikishe sheria zinazominya uhuru wa habari zinafanyiwa marekebisho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.


Naye mwezeshaji Tumaini Mbibo, amesema ni muhimu kwa waandishi wa habari kujua kiini cha matatizo yanayolikabili Taifa na njia za kutumia ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo husika.

 "Haki za binadamu zinakwenda sambamba na demokrasia hivyo uwepo wa sheria zinazominya tasnia ya habari zinakwamisha maendeleo hivyo vema ikafanyika mipango ya kufanya ushawishi wa mabadiliko" amesema.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, amesema wataendelea kuwa mstari wa mbele kupigania mabadiliko ya sheria zinazogusa tasnia ya habari kwa kushirikiana na wadau wengine.

“Tunajipanga kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kutatua matatizo yetu na yanayotukabili jamii, hatuwezi kutaka marekebisho ya sheria pasi na kushirikiana na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali” amesema.

Previous Post Next Post