WAZIRI NDUMBARO: WANAHABARI WATAKIWA KUPAMBANIA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI ZILIZOKUWA ZINABANA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI


Na Humphrey Msechu

Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF) na wadau wa Habari wametakiwa kuhakikisha wanapamba kubadili Sheria za Habari  Nchini ambazo zimekuwa zikibana uhuru wa vyombo vya Habari.

Kauli Hiyo imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro alipokutana na Uongo wa TEF na wadau wa Haki ya kupata Habari(CoRI) hivi karibuni jijini Arusha.

Waziri Ndumbaro amesema Kama Kuna wakat Mzuri wa kulisukuma suala la kubadili Sheria za Habari ni Sasa ambapo Raisi Samia ameonyesha Moyo na nia kubwa ya kutetea na kutoa Haki za vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari Nchini.

"Kwa Sasa mazingira ni mazuri yanaruhusu. Lisukumeni suala la hili la Sheria zinabadilishwe Sasa hivi, Maana mkisubiri miaka 10 ijayo, huwezi kujua atakaye kuja baada ya hapo atakuwa na matazamo gani juu ya vyombo vya Habari,"Amesema dk Ndumbaro.

Pamoja na Hayo Waziri Ndumbaro Amekubaliana na hoja ya TEF na wadau kuwa suala la Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) nchini kuwa na mamlaka ya kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka, mtoa hukumu na msimamizi wa hukumu aliyoipitisha linafifisha misingi ya utawala bora na utawala wa sheria hivyo hili ni moja ya mambo yanayopaswa kubadilishwa.

Hata hivyo, amesema kwa nia ya kusimamia na kuhakikisha haki inatendeka, ndiyo maana kilianzishwa chombo kama Mahakama ambayo ina jukumu la kusikiliza kila upande wenye malalamiko na kuamua nani anastahili haki ipi.

"Kuna hatari kubwa katika kuweka madaraka yote kwenye chombo kimoja [Mkurugenzi wa Idara ya Habari/MAELEZO…] nafahamu sheria ililenga ku-balance conflicting interests (kuweka mlinganyo kwa masilahi yanayogongana), maana serikali zote duniani huwa zinawaza kudhibiti,"Amesema.

Aidha Amemsifia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambaye ni mwanahabari na ameonyesha nia ya kusimamia mabadiliko ya sheria hizo, hivyo akashauri Jukwaa la Wahariri Tanzania na wadau kuhakikisha wanazungumza kwa karibu na Waziri Nape.

Ameahidi yeye na wabunge wengine kushiriki kikamilifu katika kusaidia Tanzania ikapata sheria nzuri za habari, kwani sheria nzuri za habari zitawezesha kukuza haki ya kupata habari, uhuru wa vyombo vya  habari na haki ya watu kutoa maoni itakayozalisha maendeleo ya haraka kwa nchi.

Kwa upande Jukwaa la Wahariri Tanzania na wadau, wanapendekeza mamlaka haya ya Mkurugenzi yafutwe na kiundwe chombo ambacho pamoja na mambo mengine kitashughulikia masuala ya usuluhishi yanapotolewa malalamiko dhidi ya chombo cha habari, badala ya kazi hiyo kufanywa na mtu mmoja.

Sheria nyingine zinazolalamikiwa ni Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Huduma za Posta (EPOCA, 2010), Sheria ya Makosa Mtandaoni (2015), Sheria ya Haki ya Kupata Habari (2016) na Kanuni za Maudhui Mtandao (2018) kama zilivyorekebishwa mara kadhaa. Sheria hizi zina vifungu vinavyofifisha uhuru wa habari nchini hivyo zinahitaji kubadilishwa.
Previous Post Next Post