TMA YAWASHAURI WAKULIMA KUPANDA MAZAO NA MBEGU ZINAZOSTAHIMILI MVUA CHACHE

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma ya Hali ya Hewa Dkt. Hamza Kabelwa akitoa mwelekeo wa Mvua za Msimu (Novemba, 2022 hadi Aprili, 2023) jijini Dar es Salaam.



Na mwandishi wetu, Dar es salaam 

Mamlaka ya hali ya hewa TMA imewashauri wakulima nchini kupanda mazao na mbegu zinazokomaa ndani ya muda mfupi na zinazostahimili mvua chache pamoja na kutumia mbinu na teknolojia za kilimo himilivu za kuhifadhi maji na unyevunyevu wa udongo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Dkt. Hamza Kabelwa wakati akitoa utabiri wa mwelekeo wa mvua za msimu kuanzia Novemba 2022 hadi Aprili 2023 ambapo sehemu kubwa ya nchi inatabiriwa kupata mvua chini ya wastani na wastani.

Hata hivyo ya Dkt. Kabelwa amesema maeneo ya Pwani ya Kusini na kusini mwa nchi mvua za chini ya wastani hadi Wastani zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Disemba mwaka huu ambapo pamoja na vipindi virefu vya ukavu itaambatana na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayoweza kuleta maafa.

"Katika Maeneo ya Nyanda za juu kusini Magharibi, mvua za wastani Hadi chini ya wastani zinatarajiwa Kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Disemba, 2022 na kuisha wiki ya nne ya mwezi Aprili, 2023," Amesema Kabelwa

Hata hivyo Amesema upungufu WA mvua unaoweza Kujitokeza Katika Maeneo mengi ya nchi unaweza kusababisha upungufu wa unyevu nyevu Katika Udongo, Chakula, malishi, ya mifugo, na maji.

Aidha Dkt. Kabelwa amesema hali ya malisho na maji kwa wanyamapori inatarajiwa kupungua kutokana na mtawanyiko hafifu wa mvua unaotarajiwa huku kina cha maji katika mito, mabwawa na hifadhi ya maji ardhini kinatarajiwa kupungua katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hali inayoweza kusababisha migogoro kati ya wanyama na binadamu pamoja na kusambaa kwa magonjwa.
Previous Post Next Post