WATENDAJI URA SACCOS WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANACHAMA


Na. Mwandishi wetu- Jeshi la Polisi, Mwanza
 
Chama cha ushirika cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (URA SACCOS)
Kimewataka watendaji wa chama hicho kutoka Mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani kutoa huduma bora kwa wanachama wake ili kuleta ufanisi na huduma za viwango vya kimataifa.
 
Hayo yamesemwa na Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP- David Misime Octoba 26 2022 ambae Pia ni Mjumbe wa Chama hicho alipokutana na Wawakilishi na Watendaji wa Chama cha hicho kutoka Tanzania bara na zanzibar wakati wa ufunguzi wa mkutano jijini Mwanza.
 


Aidha amewapongeza watendaji wa chama hicho cha kuweka na kukopa ambapo amebainisha kuwa watendaji hao wakuendelea kufanya kazi nzuri na kukifanya chama hicho kuendelea kuwa kinara kwa kutoa huduma bora nchini miongoni mwa vyama takribani 4000.
 


Chama hicho cha Ushirika cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi URA SACCOS kimehusisha watendaji kutoka Tanzania bara na Tanzania Zanzibar ambapo watendaji wametakiwa kujiimarisha katika maeneo ya utendaji wa kazi kwa kutoa huduma bora kwa wateja ili kuwavutia wateja wengi zaidi.
 


Aidha Misime ametoa wito kwa watendaji wa chama hicho kutoa huduma kulinda na mabadiliko ya kisanyansi na teknolojia ili kuongeza wingo hata kwa watejea wasio askari kujiunga nachama hicho amebainisha kuwa kikao hicho kitafanyika kwa siku mbili na mada mbalimbali zitajadiliwa ili kuleta ufanisi wa Chama cha kuweka na kukopa URASACCOS.
Previous Post Next Post