UVCCM YAWATAKA WATANZANIA KUTEMBEA KWENYE VIVUTIO VYA UTALI


Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kushiriki kwenda kwenye vivutio vya utalii lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais Mama Samia Suluhu Hassan. 

Wito umetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kata ya Mabwepande Jimbo la Kawe (UVCCM), Andrew Mashimba, wakati akizungumza na vyombo vya habari.

Kiongozi huyo alisema lengo la kuandaa matembezi hayo ya kwenda Sadaan ni kwa lengo la kumuunga mkono mama Samia katika jitihada zake za kutangaza utalii wa Nchi yetu.

Alisema ni vyema watanzania tukapenda vya kwetu kuliko kunyamaza kimya na kuishia kulalamika.

Katibu wa UVCCM Mabwepande Ramadhani Kindamba alisema kuwa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha jambo hili linatimia.

"Sisi tukiwa vijana lazima tumuunge mkono mama na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa hivyo uchaguzi umeisha na sasa kazi 'Iendelee'.


Previous Post Next Post