TATHMINI YA MIPAKA YA MAPORI YA AKIBA YALIYOPANDISHWA HADHI MKOANI KATAVI HAITAINGILIA MAAMUZI YA BARAZA LA MAWAZIRI




Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema kuwa tathmini ya mipaka mipya ya Mapori ya Akiba yaliyopandishwa hadhi na kuonekana kuwa na changamoto ya muingiliano wa mipaka, haitagusa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu mipaka ya vijiji. 

Ameyasema hayo Oktoba 12, 2022 mkoani Katavi wakati wa Ziara ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya Ardhi katika vijiji 975 nchini.



“Mwaka 2021 Wizara ya Maliasili na Utalii ilipandisha hadhi mapori matano ikiwemo Tongwe East kutoka pori tengefu kwenda pori la akiba lakini wataalam walipoingia uwandani wakagusa maeneo mengine ikaonekana kuna muingiliano wa mipaka” Mhe. Masanja amefafanua.

Amesema kutokana na changamoto hiyo,Waziri wa Maliasili na Utalii aliunda Kamati ya kushughulikia suala hilo na hatimaye ilikuja na tamko kwamba mipaka ya maeneo yaliyokosewa itarekebishwa na kusisitiza kwamba haitagusa vijiji ambavyo vimefanyiwa maamuzi na Baraza la Mawaziri.



“Tathmini ilivofanyika ilibaini kuwa Hifadhi ya Msitu ya Mpanda Line, Tongwe West, Sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Masito, Eneo la Makazi ya Wakimbizi la Mishamo, Sehemu ya Maeneo ya Vijiji katika Kata ya Mishamo viliingizwa vyote kwenyePori la Akiba la Tongwe East lakini lengo ilikuwa ni kupandisha Pori la Akiba la Luganzo Tongwe.

Ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta itaendelea katika mkoa wa Kigoma tarehe 13 Oktoba 2022.
Previous Post Next Post