HOSPITAL YA CCBRT YAPOKEA MSAADA WA MASHINE YA ULTRASOUND KUTOKA KAMPUNI YA SWISSPORT



Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Kampuni ya kuhudumia Mashirika ya Ndege, Abiria na Mizigo Katika viwanja vya Ndege (Swissport) imewakabithi mchango wa Mashine ya  Ultrasound ambayo itatumika kuwasaidia kina Mama wajawazito  Katika Hospital ya CCBRT yenye thamani ya shilingi Milioni 63.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijin Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport, Mrisho Yassin amesema wanatambua kama Kuna Changamoto wa vifaa vya Tiba hasa Katika kitengo Cha Wajawazito Katika Hospital ya CCBRT.

"Kwa taarif tulioyopewa itasaidia sana Kwa Sababu ni Mashine Ambayo inatajika hapa CCBRT na sisi tunawshukuru na tunafurahi tukiamini Mashine hii inatutumika na mchango wetu Katika jamii utatumiwa ipasavyo kusaidia jamii ya kitanzania hasa kina Mama wajawazito" amesema  Mrisho Yassin.


Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Bi Brenda Msangi amesema wanawashukuru Swissport Kwa kuona umuhimu wa kuchangia huduma wanazotoa Kwa kina Mama Kwa vifaa Tiba Kama Ultrasound walioitoa Ambayo itawezesha  kuwahudumia kina Mama wajawazito wengi Zaidi.

"Nichukue Fursa hii kuifahamisha hadhara hii kuwa tangu kuanza kutolewa Kwa Huduma Katika kitengo chetu Cha Mama na mototo mwezi Januari  Hadi oktoba 2022 tumeweza kuwahudumia akiba mama wapatao 225" Amesema Brenda Msangi.

Bi Brenda Amewaasa wanawake wajawazito walioko Katika kundi Maalumu na  wanawake Wengine wote kudhuria kliniki Mara wanapojingundua kuwa wajawazito ilikuweza kufuatilia Maendeleo ya Afya na ujauzito.
Previous Post Next Post