MAKAMU WA RAIS PHILIP MPANGO MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA MAONYESHO YA SITA YA S!TE


Na Lilian Ekonga, Jijin Dar es salaam 

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe Philip Mpango anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi Katika ufunguzi wa Onesho la sita la Swahili International Tourism Expoo (SITE) ambalo litafanyika Katika Ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21 Hadi 23 Oktoba.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Felix John, Amesema Onesho Hilo lita huudhuriwa na wafanyabiashara za Utalii kutoka ndani na nje ya nchi ambao watapata fursa ya kuonyesha bidhaa mbalimbali za Utalii, kutengeneza mtandao wa biashara, kuanzisha na kuimarisha mahusiano ya biashara.

"Tangu kuanzishwa Kwa S!TE mwaka 2014, Onesho Hilo litakuwa na mafanikio makubwa ikiwemo Ongezeko la waoneshaji na wanunuzi wa kimataifa ambao wamekuwa wakiongezeka Mwaka Hadi mwaka"

Alikadhalika Felix amefafanua kuwa maonyesho haya yatahusisha utangazaji WA bidhaa mbalimbali za Utalii, jukwaa la uwekezaji, Semina kuhusu masuala ya utalii na masoko zenye Lengo la kuwajengea uwezo wadau.

Aidha amesema Onesho hill litahudhuriwa na waoneshaji Zaidi ya 200 na wanunuzi wa kimataifa takribani 100 kutoka Katika masoko yetu ya utalii ya kimkakati hususani nchi za Marekani, Uholanzi, Afrika kusini, India na Urusi.

Felix ameongeza kuwa Onesho la S!TE 2022 ni sehemu ya jitihada za kuiendeleza Programu Maalum Tanzania ya The Royal Tour iliyo sisiwa na RAIS Samia Suluhu Hassan yenye Lengo la kutangaza vivutio vya Utalii na fursa za uwekezaji zilizopi Nchini.

"Naomba kutoa Rai Kwa wadau wa Utalii waliopo ndani na nje ya nchi hususani Wakala wa biashara za Utalii, watoa Huduma za Makazi, Wakala wa safari na waongoza watalii kuchangamkia fursa za kiuchumi na kijamii zitakazotokana na Onesho la S!TE 2022"

Kwa upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo , Heri James amesema Serikali inawahakikisha usalama wa kutosha Katika Onyesho Hilo la S!TE na kuwaasa wananchi Kujitokeza Kwa wingi Katika Maonyesho hayo.

"Onesho la S!TE 2022 limedhaminiwa na wadau mbali mbali Katika sekta ya Utalii wakiwemo Mamlaka ya Bandari (TPA) ambae ndio mdhamini Mkuu wa jumla Vodacom Tanzania ambao ni washamini wakuu upande wa mawasiliano na Huduma za Fedha kupitia Huduma yao ya M-PESA, Kampuni ya ONA&METAS, CRDB , TATO na wengine"

Huku kauli Mbiu ikiwa Kuupeleka Utalii Katika Ngazi za Juu
Previous Post Next Post