MABADILIKO YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YATAIPA HESHIMA SEKTA YA HABARI


Na Humphrey Msechu

Mabadiliko ya vipengele vya Sheria ya Huduma za Habari yataipa heshima sekta ya Habari na kuongeza chachu ya uwajibikaji kwa kutunza misingi, miikona maadili ya kitaaluma.

Pia waandishi wa habari nchini wametakiwa kuweka mazingira ya matumizi ya mitandao ya kijamii vizuri kwa kuipa kipaumbele katika usambazaji wa taarifa hasa zinazohusu kampeni ya utetezi mabadiliko ya sheria ya habari ya mwaka 2016 ambayo wadau wa habari wamekuwa wakilalamikia baadhi ya vifungu kandamizi kwenye sheria.


Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Deodatus Balile kwenye Semina ya Siku moja na Waandishi wa habari ambayo ililenga kufanya mapitio ya utendaji wa TEF katika mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari ya mwaka 2016 ikiwa ni sehemu ya kufunga mradi wa kufanya uchechemuzi kwenye mabadiliko ya sheria hiyo.

" Waandishi wa kipindi mna faida kubwa sana ya uwepo wa mitandao Kijamii ikitumika vizuri inaweza kuleta mabadiliko katika jamii kutokana na habari mnazoziandika , siku hizi ukiwa na simu janja unaweza kufanya kila kitu na ujumbe wako ukafika kwa jamii " amesema Balile


‘‘Tunapaswa kuwa na stori ambazo hata hapo baadaye, wengine watakaokuja watajua kuna kazi iliyofanywa" 

Katika hatua nyingine Balile amewashukuru wanahabari hao kwa kazi kubwa mrejesho walioutoa kwa kuandika habari zinazohusu kampeni ya utetezi wa sheria ya vyombo habari nchini huku kusisitiza uendelevu na ushirikiano wa waandishi na Wahariri ili kufanikisha kampeni hiyo .
Previous Post Next Post