CHAMA CHA NRA KIMEPINGA UCHAGUZI FEKI ULIOFANYIKA SEPTEMBER 24, 2022


Na Lilian Ekonga 

Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA) kimepinga Uchaguzi Feki ulioitishwa na kufanyika Septemba 24,2022 mkoani Morogoro na aliyekuwa Katibu Mkuu wake Bw.Khassani Kisabya Almas sambamba na aliyekuwa makamu Mwenyekiti kwa upande wa Zanzibar Bw.Khamis Faki Mgau.

Akizungumza na waandiishi wa habari wakati akitoa taarifa ya kutotambua uchaguzi huo, Mwenyekiti wa NRA Taifa, Bw.Simai Abdalla amesema sababu za kupinga uchaguzi huo ni pamoja na kuitishwa tofauti na Mamlaka za uitishaji wa Mikutano ya uchaguzi wa viongozi wa chama ngazi ya Taifa.


Amesema Mkutano Mkuu haukuwa na wajumbe halali kwa zaidi ya 65% badala yake walitaffutwa wajumbe ambao hawatambuliki kutoka mkoani Morogoro na kuweza kushiriki mkutano huo.

“Mkutano huo haukusimamiwa na Kamati ya Chama ya Uchaguzi badala yake ndugu zake Khassan Kisabya Almas na Mohamed Abood Mgombea Uwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ndio waliosimamia”. Amesema Bw.Abdulla.

Nae Makamu Mwenyekiti wa NRA Taifa, Bi.Mariam Olutu amesema tayari wameshamuandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu suala la kutokubaliana na uchaguzi huo na baadae wataenda Mahakamani ili haki iweze kutendeka.


Hata hivyo spark light blog ilifanya jitihada za kumtafuta Katibu Mkuu Bw.Khassani Kisabya Almas kwa njia ya simu kwa zaidi ya mara tatu huku simu yake ikiwa hapokelewi

 Jitihada zaidi za kumtafuta bado zinaendelea kufanyika.
Previous Post Next Post