BALILE: Baadhi ya vifungu vya sheria ya habari vinawabana waandishi

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile akimkaribisha Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt.Wiebe de Boer ili kufungua kikao kazi cha wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na waandishi wa habari kinachofanyika kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam leo.


Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt.Wiebe de Boer akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile kushoto na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Bakari Machumu kabla ya kufungua kikao kazi cha Jukwaa la Wahariri na waandishi wa habari kinachojadili sheria ya habari leo Alhamisi Oktoba 20, 2022 kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.

Anita Mendonza Afisa Mtendaji Mkuu Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF akifuatilia kikao hicho kinachofanyika kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam pamoja na Elizaberth Chanzi mmoja wa maofisa wa TEF.

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt.Wiebe de Boer akiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile kushoto na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Bakari Machumu pamoja na baadhi ya wajumbe mara baada ya kufungua kikao kazi cha Jukwaa la Wahariri na waandishi wa habari kinachojadili sheria ya habari leo Alhamisi Oktoba 20, 2022 kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.


Na Humphrey Msechu

Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) ndugu Deodatus Balile ameshauri baadhi ya sheria za habari zinawabana waandishi wa habari na kushidwa kufanya kazi kwa weledi lakini pia zinawabana na kushidwa kutetea haki na maslahi yao huku akitolea mfano vyuo vingi vya Africa vinafundisha waandishi wa habari kutetea jamii huku akisema katika mafunzo hayo hamna sehemu inamwambia mwandishi kwamba naye ni mmoja wa kundi linalotakiwa kutetewa kitu ambacho kinafanya waandishi wengi kushidwa kujieleza kuhusu matatizo wanayokutana nayo katika kazi zao.

Baadhi ya taasisi zinadai kutetea haki za waandishi wa habari lakini hawajui chochote kuhusu changamoto hizo ndio maana sisi Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) tukasema tuanze kutetea haki na maslahi ya waandishi wa habari , Sisi ndio tunafanya kazi za habari ndio tunajua changamoto tunazokutana nazo hivyo sisi ndio tunaweza kujieleza na kutetea haki zetu ili duniani itambue na tupate namna ya kutatua changamoto hizo,
Amesema.

Ndugu Deodatus amendelea kusema baadhi ya vifungu vya sheria ya habari vinawabana waandishi hivyo wapo kwenye michakato kuwaomba watunga sheria ili vifungu hivyo vifanyiwe marekebisho au kubadilishwa hasa vile ambavyo vimekuwa kikwazo kwa kazi za wanahabari.

Aidha Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe De Boer akifungua kikao kazi hicho amepongeza Jukwaa la Wahariri TEF katika programu zao za kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kufanya kazi kwa weledi zaidi na ameongeza kuwa sema ubalozi wa Uholanzi uko tayari kusaidiaTEF katika mipango yake. 
Previous Post Next Post