IGP WAMBURA APANGUA BAADHI YA MAKAMANDA POLISI


Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura, amewahamisha baadhi ya
Makamanda wa Polisi kutoka katika nafasi zao na kuwapangia sehemu zingine.

Amempangia Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei, kuwa
Mkuu wa Kitengo cha Polisi Wasaidizi na Kampuni Binafsi za Ulinzi nchini ambapo
anachukuwa nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Issack Katamiti.

Pia, amewahamisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani
Ng'anzi, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ambaye amehamishwa
kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania na aliyekuwa Mkuu
wa Kikosi hicho Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad
Mtafungwa, anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.

Naye, aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Kipolisi Rufiji Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP) Protus Mutayoba, amekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rufiji baada
ya Kamanda wa Mkoa huo kuhamishiwa Mkoa wa Kipolisi Temeke hivi karibuni.
Previous Post Next Post