WAZIRI MABULA: TAASISI ZA FEDHA ZIONGEZE WIGO WA UTOAJI MIKOPO YA NYUMBA KWA WANANCHI WENYE KIPATO CHA CHINI



Waziri wa Ardhi  Nyumba na Maendeleo ya makazi , Angelina Mabula ametoa wito Kwa Benki Kuu ya Tanzania Kwa kushirikiana na Benki na tasisi za fedha kutafuta mbinu za kutatua  Changamoto ya upatikaji wa mikopo yenye riba nafuu Ili kuwawezesha wananchi kumudu gharama za mikopo hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi  wa Mkutano wa wadau wa uendelezaji Milki amsema Taasisi za Fedha ziongeze  wigo wa  Utoaji wa mikopo ya nyumba Ili kuwawezesha  wananchi wenye kipato Cha chini ambao ndio wengi Nchini Kupata fursa ya Kupata mikopo ya nyumba.

"Mbali na mikopo ya nyumba, niziombe Benki Nchini kutoa mikopo Kwa ajili ya kukamlisha zoezip0. la urasimishaji linalotarajiwa kukoma 2023" amsema waziri Mabula.

Pia Waziri Angelina amesema nchi yetu inakadiriwa kuwa na upungufu wa takribani nyumba Milioni 3 naongezeko la mahitaji ya wastani  wa takribani nyumba 200,00 Kila mwaka.

Amsema Takwimu zinaonesha kuwa kuanzia mwaka 2010-2022 tasisi kubwa 8 zinefanikiwa Kujenga nyumba takribani 13,837 sawa na wastani wa nyumba1,153 Kwa mwaka.

Aidha amsema zoezi la sensa ya watu na makazi linaloendelea Nchini litawezesha Serikali kuwa na kanzidata ya nyumba zote Nchini, hivyo Kupata Takwimu sahihi za upungufu wa nyumba Nchini pia itafungua fursa Zaidi ya kujua mahitaji halisi ya nyumba  Kwa Kila mwaka.

Hata hivyo waziri Mabula amewahimiza wadau kutoka katika Kila sekta milki kufuata mbinu zinazofaa Katika kuepuka na kukabiliana na atahari za mabadiliko ya tabaia ya nchi.

"Nichukue fursa hii kuhimiza Taasisi zinazojihusisha na uendelezaji Milki kujikita Katika dhana ya ujenzi wa kijani utakowezesha utunzaji wa mazingira lakini pia unapunguza matumizi ya vifaa vinavyozalisha gesi zinazo ongeza madhara kwenye Hewa ambazo husabbisha tatizo la mabadiliko ya tabaia ya nchi"amsema waziri Angelina Mabula
Previous Post Next Post