WAZIRI MABULA AWASHUKIA WANAOCHOCHEA NA KUCHONGANISHA SERIKALI NA WANANCHI



Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Daktar Angeline mabula amesema serikali itahakikisha inafanya mabadiliko ya sera na sheria za Milki ili kuhakikisha kunakuwepo na miji na makazi bora yalipongika vizuri na yenye usalama na miundombinu yote Muhimu ikiwemo maji, barabara na umeme.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akifunga mkutano wadau wa milki nchini ambapo amesema wizara itaweka utaratibu mzuri wa kuendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau na wananchi ili kuwepo na mabadiliko ya kasi katika sekta hiyo.

“Sekta ya milki ikitumika vema ni sehemu ambayo itazalisha ajira nyingi zaidi,itakuza uchumi kutoa manufaa makubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla”

Ameongeza kuwa mkutano huo ulihudhuliwa na washiriki wapatao 230 huku wengine wakifuatilia kupitia Runinga na mitandao mbalimbali ambapo mada nane ziliwasilishwa na kujadiliwa kwa pamoja na kupokea maoni.

Aidha Dkt mabula amewataka watu wenye tabia ya kuchochea na kuchonganisha serikali na wanachi kuacha tabia hiyo kwani inasababisha kudhorota kwa mausiano baina ya pande hizo mbili

“Jana hapa nilizizungumzia kuhusu kupiga marufuku uuzaji viwanja 20 kwa 20 kwenye miradi ya uuzaji wa ardhi watu wanajitokeza kwenye mitandao na kusema serikali haitaki watu wakipato cha chini kunufaika kupitia miradi hiyo wakati sio kweli”

“Serikali inapinga hilo kwa kulinda maslai ya wananchi wanasema wanauza kusaidia wananchi wakipato cha chini laki ukiangalia bei yake ni ghali unakuta kiwanja ni 20 kwa 20 lakoni kinauzwa zaidi ya milion 10 hakuna huduma za kinamii,hakuna barabara zenye mapana sasa hata ukitaka kupitisha huduma za maji na umeme inashindikana sasa unakuwa umemsaidia mwananchi ama umemwangamiza”

Dkt mabula ameendelea kwa kubainisha kuwa serikali inataka kuwepo na makazi bora yenye nafasi na yalipangika vizuri kwa uuzaji wa viwanja vidogo hilo halitafanikiwa.

Sambamba na hayo amewataka watu wenye maeneo katikati ya mji na kuyaacha kuwa mapori kuhakikisha wanayaendeleza,naendapo watasgindwa kufanya hivyo serikali itayafutia hati na kuyagawa kwa wawekezaji wengine wenye nia.
Previous Post Next Post