Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na makundi Maalumu Dkt, Dorothy Gwajima amefanya halfa fupi ya kumuag mtoto Victor Paschal Ntatau ambaye ni mjumbe wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Baraza la Watoto la Mkoa wa Singida anayekwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mkutano wa Dunia wa Watoto utakaofanyika katika Jiji la Billund nchini Denmark kuanzia tarehe 13-16 Septemba 2022 .
Akizungumza na waandishi waandishi wa habari waziri gwajima Amesema anapenda kumshukuru Katibu Mkuu na timu yake ya wataalam wa Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008 inayohimiza ushiriki wa mtoto katika masuala mbalimbali hasa ya kijamii.
Waziri Amsema Katika kuimarisha ushiriki wa Watoto nchini, Serikali iliandaa Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya Mwaka 2008 na katika Sura ya 5 imetoa maelekezo kwa wadau kuhakikisha kuwa Watoto wanashirikishwa katika masuala yanayowahusu.
"Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wazazi wa mtoto Victor kwa kumpa nafasi mtoto kushiriki katika mabaraza haya, na kipindi chote cha usaili mtandaoni ambao naambiwa umechukua takribani miezi sita (6) ambapo amefanya usaili mara sita tofauti na hatimaye kuibuka mshindi kwa nchi yetu na kati ya watoto saba (7) waliochaguliwa katika Bara la Afrika ambaye atajumuika na watoto wenzake wapatao 80 kutoka nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa" Amesema waziri Gwajima.
Pia Waziri ametoa wito kwa wazazi na walimu kuwaruhusu watoto kushiriki katika shughuli za mabaraza kwa kuwa yana manufaa sana katika kuimarisha uwezo wa watoto kuweza kujieleza, kujiamini na kutafakari mambo na kujilinda katika hatua za malezi na makuzi yao
Kwa upande mwingine Waziri Gwajima ememkabidhi amemkabidhi Bendera ya Taifa, Mtoto Victor Ili kuliwakilisha Taifa katika Mkutano wa Jukwaa la watoto Duniani.
Aidha waziri ameagiza watendaji wake kupitia Katibu wa Wizara kuhakikisha Mtoto Victor kipaji na uwezo wake unaendelezwa ili kufikia malengo ya makuzi na utimilifu katika maisha yake ya utoto na hatimaye kuwa raia mwenye tija anapokuwa mtu mzima.
" Naagiza Wizara kupitia Idara ya Watoto kuandaa kikao cha baraza la watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mambo mengine ili Mtoto Victor aweze kuwasilisha maazimio ya kikao atakacho hudhuria"amsema Waziri Gwajima.
Kwa upande wa Baba mzazi victor amesema wanamshukuru Serikali kupitia Baraza la watoto la mkoa wa singida kumumsaidi mtoto wao kuweza Kupata nafasi ya kuwakilisha nchi na kumjengea uwezo.
"Victor aliweza kushiriki na kuzungumza maswala yote atakayokwenda kuzungumza Denmark na tunawshukuru aliweza kumudu" amsema baba wa Victor.