Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka (kulia) akiwa na Mhe. Balozi Maimuna Tarishi kutoka Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva wakiwa katika Mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu unaendelea Geneva, Uswisi, ulioanza tarehe 12 Septemba na utaendelea hadi tarehe 7 Oktoba 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akiteta jambo na baadhi ya Wajumbe wasaidizi wake katika Mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu unaendelea Geneva, Uswisi, ulioanza tarehe 12 Septemba na utaendelea hadi tarehe 7 Oktoba 2022.
Na. Mwandishi Wetu, Geneva.
UJUMBE kutoka Tanzania unashiriki mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu unaendelea Geneva, Uswisi ambapo Tanzania inatarajiwa kuwasilisha ajenda mbalimbali ikiwemo Haki ya Maendeleo kwenye Elimu,Afya, Makazi, Maji salama, Usafi na mengine ikiwemo UVIKO19 katika sekta ya Utalii.
Ujumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka unahudhuria mkutano huo vikiwemo vikao vya pembezoni
Wajumbe wengine kwenye mkutano huo ni pamoja na Mhe. Balozi Maimuna Tarishi kutoka Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva.
Mkutano huo umeanza rasmi tarehe 12 Septemba 2022 na utaendelea hadi tarehe 7 Oktoba mwaka huu.
Aidha, katika Ajenda hizo ambazo zinatarajiwa kuwasilishwa suala la athari za Uviko 19 hasa katika sekta ya Utalii litazungumziwa kwa kina mikakati madhubuti iliyowekwa ya kudhibiti uchumi dhidi ya janga hilo, ikiwemo kuhimiza utoaji wa chanjo ya UVIKO19 na kutangaza Nchi kupitia Royal Tour, ambayo imeleta matokeo chanya yaliyopelekea watalii kuongezeka kwa kiwango kikubwa.
Nchi mbali mbali zinashiriki mkutano huo wa 51 huku zikitarajiwa kuwasilisha ajenda za kimaendeleo ya Mataifa yao.