NA MWANDISHI WETU
Mzee Ramadhan Rashid mwenye umri wa miaka 80, mkazi wa wilayani Kisarawe, amekuwa mmoja kati ya watu 300, waliojitokeza kuanza shule ya awali inayotolewa kupitia mpango wa elimu ya watu wazima MUKAJA na ule wa waliokua nje ya mfumo rasmi wa elimu MEMKWA.
Mzee Ramadhan, amejiunga na wenzake zaidi ya 300 waliokua hawajui kusoma, kuandika na kuhesababu kabisa, kwa lengo la kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Mzee Ramadhan amesema, amefikia hatua hiyo kutokana na changamoto aliyokuwa akikumbana nayo hasa wakati wa kusoma mikataba ya mauziano ya mashamba, hali iliyompelekea kurudi darasani kupata elimu hiyo.