Na Humphrey Msechu, Geita
Katibu mkuu wizara ya madini Adolfu Ndunguru amewataka wawekezaji nje na ndani ya Tanzania kuja kuwekeza katika sekta ya madini na waje na mitaji yao.
Hayo ameyasema wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya maonesho ya 5 ya madini ya kitaifa ya tekinolojia ya madini 2022 mkoani Geita yenye kauli mbiu madini ni fursa za uchumi, ajira kwa maendeleo endelevu.
Amesema kuwa matarajio ni makubwa sana kwani baada ya maonyesho hayo uwekezaji kwenye sekta hiyo utaimalika hivyo maonyesho yameaza leo na niwakati sasa watanzania na wasio watanzania wajitokeza kwa wingi ili kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji katika eneo la madini.
"Amesema nimekuja kukagua maendeleo ya maandalizi ya maonyesho ya madini ambayo yameaza leo hivyo mambo yanaenda vizuri kama mnavyoona hivyo ni matarajio yangu nikuona kuwa wananchi wa mkoa wa Geita na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho haya maana ni fursa kwao kwa wafanyabishara ndogo ndogo ”alisema katibu mkuu Ndunguru
Amesema upatikanaji wa miundombinu kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wadogo ikiwemo umeme maji na mambo mengine Amesema wizara ya madini imejipanga vizuri kusaidia wachimbaji wadogo na kwakuliona hilo waliwapatia mlezi ambaye ni Shirika la madini la Taifa (STAMICO) ndilo linawawezesha kutambua fursa zilizopo na kuwakutanisha na mabenki kwa jailli ya kuwapatia mtaji ili waweze kuwapatia msaada.
Amesema kuwa kuhusu umeme wao kama wizara ya madini wanakaa na wizara ya Nishati ili kuona umeme unafika maeneo mengi zaidi nchini na sio tu kwenye upande wa madini bali hata kwenye sekta zingine waweze kuwafikia na kwamba wanamkakati wa kupeleka umeme kote nchini.
“Tunamkakati wa kupeleka umeme nchi nzima kwa wachimbaji wadogo ,wazalishaji wa mazao kwahiyo wizara jukumu lake nikuwasiliana na sekta husika ,ili kuweza kufikiwa hawa watu na kuwapatia huduma kwa maendeleo ya nchi.”amesema