KUNA WASANII WANAKURUPUKA KUTUNGA NYIMBO ZA TOZO, BASATA ISIRUHUSU NYIMBO HIZO ZA UPOTOSHAJI


Msanii wa Bongo Steve Nyerere amewasihi Watanzania kuendelea kuchangia kodi kupitia tozo za miamala ya benki na simu kwa madai kuwa tozo hizo zinasaidia  kuleta Maendeleo Kwa Taifa.

 Hayo ameyasema leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari amesema  jambo la tozo lipo duniani kote nakwamba ni Jambo ambalo la tija kwa Taifa kutokana na kutatua changamoto mbalimbali za Maendeleo Kwa wananchi.

 Aidha amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inataka kuwafikisha watanzania kwenye hatua ya Maendeleo ya kujivunia wenyewe hivyo na kuondokana na kutegemea hisani kutoka mataifa ya nchi za nje ikiwemo Ulaya na Asia.

 " Tozo hizi zipo duniani kote,tusiwekeze siasa na Kodi, watanzania wote tujivunie na tozo zilizopo ,kama tozo hii ina problem( tatizo) kidogo inaweza kusawazishwa tu na mambo yanaendelea na siyo kuiondoa kabisa" amesema Steve.

 Amesisistiza kuwa tozo hizo zinasaidia kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo kujenga Barabara ,Madaraja,Reli ya Kisasa,Hospitali ,na miradi mingine ya maendeleo,hivyo watanzania wanapaswa kushikamana na serikali katika kutekeleza Ujenzi wa miradi hiyo kupitia tozo.

 Ameongeza kuwa endapo Watanzania watekeleza tozo hizo watakuwa wameonyesha uzalendo wa hali ya juu nakwamba hata nchi zingine zilizoendelea akitolea mfano China, Singapore,na Malasia zinategemea kodi kutokana na tozo.

 "Kuna wengine tumewaona wanaenda Mahakamani kupinga tozo hizi,pia kuna wasanii wanakurupuka kutunga nyimbo za tozo nimezungumza na BASATA isiruhusu nyimbo hizo za upotoshaji,kwani uhuru tukiuruhusu sana utatugawanya" amesema.

 Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwaomba Viongozi wa Dini,Wanasiasa,na Waandishi wa habari kuelimisha Jamii kuhusu umuhimu wa  tozo zinazotozwa kwenye miamala ya kibenki na simu ili kuondoa sintofahamu Kwa wananchi.
Previous Post Next Post