GF TRUCK KUTOA FURSA KWA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO


Na Humphrey Msechu, Geita

MENEJA Masoko na Mawasiliano kutoka kampuni ya GF Truck Group, Smart Deus amesema kuwa kupitia maonyesho ya tano ya kitaifa ya madini ya mwaka huu 2022 yanayofanyika mkoani geita wamekuja na mpango wa kuchangia damu salama na kutoa zawadi mbalimbali kwa  watakaoshiriki kushiriki kutoa damu.

Deus ameyasema hayo leo Septemba 27 mwaka huu katika viwanja vya maonyesho ya madini mkoani humo mara baada ya kutembelewa na mkuu wa wilaya ya geita Wilson Shimo.


Amesema kuwa katika maonyesho ya madini kwa mwaka huu wao kama Gf Truck group  na Damu salama watakuwa na huduma ya uchangiaji damu kama sehemu ya mchango wao kwenye jamii.

Amefafanua kuwa  katika uchangiaji huo wa damu  watatoa zawadi za tisheti  lakini kwa upande wa  waendesha piki piki (bodaboda) watatoa  vizibao na hiyo yote ni katika kutoa hamasa  kwa ajili ya kuchangia damu.

Katika hatua nyingine Meneja Deus amesema kuwa kwa mwaka huu wameingia makubaliano ya kusaidia timu ya mpira wa miguu Geita fc ambayo ni timu inayotoka katika mkoa huo hivyo wanategemea hata wao kushiriki katika zoezi la kuchangia damu.


Pia ameongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na ofa kwa wale watakao nunua  gari au mashine watapewa zawadi mbili moja ikiwa pamoja na kutembelea hoteli yao iliyopo wilayani bagamoyo kwa siku tatu yeye na familia yake na pia zawadi nyingine ni watafanyiwa  huduma ya matengenezo kwenye mashine ama gari kwa mwaka mzima.

Deus alimaliza kwa kushukuru mkoa na wilaya ya geita kwa ushirikiano wao na hata wadau wa madini kwa kuendelea kutumia bidhaa zao za Gf truck group.

Na Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Gf Truck Paul Msuku amesema katika kusaidia wachimbaji wadogo mashine walizonazo mteja anaweza kutanguliza kiasi cha malipo na baadae analipa kidogo kidogo mpaka pale atakapomaliza deni lake.


Amesema kuwa ni nisehemu ya mchango wao katika kumupunguzia mzigo mchimbaji mdogo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo amesema kuwa wanashukuru mchango wa Gf Truck wanaoutoa katika mkoa wa geita  huku akiwataka pia kuwekeza pia kwa upande wa hoteli maeneo ya fukwe zilipo mkoani humo ikiwemo Nkome na kwingineko.
Previous Post Next Post