WAZIRI MKENDA MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA TATU YA GLOBAL EDUCATION LINK.



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda  anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi Katika Mahafali ya Tatu ya Wakala wa vyuo vikuu vya nje ya nchi (GLOBAL EDUCATION LINK) yatakayofanyika Tarehe 21 mwezi 8 Katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar esa salaam kuanzia saa nne kamili Hasubuhi.

Hayo yamesemwa leo Agosti 18 na  Mkurugenzi Mtendaji wa Global Educational Link Ltd, Abdulmalik Mollel amsema mahafali haya Yana wahusu wanafunzi wa kitanzania walio hitimu vyuo vikuu vya nje ya nchi. 

" Kama tunavyofahamu sio wanafunzi wengi walio fanikiwa  kuhitimu masomo yao kutoka na Janga Zima la UVIKO-19  na kunabadhi ya nchi zilifungua mipaka na Kuna Baadhi ya nchi zingine zilifungua mipaka yao Ila vijana wetu Kwa Baadhi ya kozi kama udaktari walikuwa wapo kwenye kipindi Cha mafunzo."amesema Mollel

Amsema Malengo ya mahafali haya ni kukutanisha wanafunzi Hawa pamoja na wazazi wao kusherekea Kwa pamoja WAKIWA hapa nyumbani na tunakutanisha wanafunzi waliomaliza nchi mbalimbali.

Mollel amsema Lengo la pili ni Kujenga daraja Kwa wanafunzi pamoja na Taasisi mbalimbali ambazo zinazohitaji kutoa AJIRA hasa wanapoitaji vijana walio soma nje kwa sababu waajili wengi hutuma barua za kuhitaji vijana Hawa  Kwa GLOBAL EDUCATION LINK.

"Tunategemea kuwa na wahitimu 400 ambao wamepeta nafasi  kutokana na Ukumbi  nao hauwezi kuwamudu wanafunzi wote hivyo tumechukua wanafunzi wachache"amsema Mollel 

Aidha amsema wamealikwa wazira mbali mbali ikiwe wizara ya Elimu , Wizara ya Mambo ya nje na wizara ya kazi na vijana na wizara ya Afya ikiwemo ya wizara ya Elimu Zanzibar. 
Previous Post Next Post