TRA YAZIDI KUTOA ELIMU YA KULIPA KODI KWA HIYARI



MAMLAKA ya mapato mkoa Mbeya (TRA) imesema kuwa kumekuwa na ongozeko la ulipaji kodi kwa hiyari hasa upande wa kilimo kutokana na kutatua migogoro nje ya mahakama.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya mapato Mkoa wa Mbeya(TRA)Nuhu Suleiman wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati waliyoweka kwa walipa kodi katika kipindi hichi cha maonyesho ya wakulima Nanenane ambayo kitaifa inafanyika mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale Jijini hapa.

Suleiman amesema kuwa kitu kingine kinacholeta msukumo wa hiyari kwenye ulipaji kodi ni usikilizaji wa malalamiko kwa walipa kodi. 

"Ni kweli suala la kodi linahusu kila mwananchi na wakati mwingine kuna kuwa na changamoto ya nguvu kazi lakini sasa hivi tunaishukuru serikali na pia tunashukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwasababu tumeongozewa watumishi 2000 kwa hiyo sisi watumishi tumejipanga kwenda maeneo ambayo yamejitenga na mji kwa ajili kusambaza elimu"amesema. 



Aidha Kaimu Meneja huyo amesema kuwa katika maonyesho hayo pia kutakuwa na fursa kwa wawekezaji3 kuweza kuelewa bidhaa ambazo zipo kwenye misamaha ya kodi. 

Hata hivyo Suleiman amesema kwa suala la kodi ni muhimu na kwamba nchi haiwezi kwenda bila ulipaji wa kodi hivyo elimu itaendelea kutolewa kwa wananchi ili waweze kuendelea kulipa kodi. 

Fatum Mohamed ni mjasiliamali wa Duka la Nguo Soweto amesema hivi sasa ulipaji wa kodi unaenda heshima kubwa sana kwani tunalalamika wenyewe. 

"Wengi tumebadilika kutokana na TRA kutoa elimu mara kwa wananchi ndo unakuta hata kwenye maonyesho tunajitokeza kwa wingi"amesema.


Previous Post Next Post