TIC YATAJA VIPAUMBELE VYAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2022-2023



Serika ya Awamu ya Sita Chini ya Uongozi Mahili wa Rais Mama Samia Suluhu Hassani imedhamilia kuendelea kuwa vutia wawekezaji hapa nchini ili kusadia Watanzania kunufaika na Ajira zitakazo weza kupatikana.

Hayo yamesemwa leo  Jijini Dar es salaam na  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania TIC, Bwana John Mnali wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  na mwelekeo wa Utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022-2023 .

Mnali amesema TIC imepata mafanikio makubwa kutokana na kuimarika kwa shughuli za utaratibu na utoaji wa huduma kwa wawekezaji kupitia utoaji wa huduma mahala pamoja ndani ya TIC na hivyo kusaidia ongezeko la usajili wa miradi.

Ameongeza kua katika kipindi cha mwezi Juni 2021 hadi Julai 2022 jumla ya miradi 274 imesajiliwa ikilinganishwa na miradi 234 iliyosajiliwa katika kipindi hicho mwaka 2022/2021 ambayo ni sawa na ongezeko la asimilia 14.6 



Kuhusu vipaumbele vya Kituo Cha Uwekezaji Tanzania TIC na mwelekeo wa Utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2022-2023 Mnali amesema kituo hicho kitaendelea kuboresha na kuimarisha huduma zitolewazo katika kituo cha huduma mahali pamoja ( One Stop Facilitation Centre) ili kufanikisha Uwekezaji.

Vilevile Mnali amesema TIC itaendelea kufanya tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na tafiti za kuibua fursa za Uwekezaji nchini , tafiti za kuboresha mazingira ya Uwekezaji, tafiti za kuibua maeneo yenye fursa za uwekezaji kwaajili ya wajasiriamali wa kati na wadogo.


Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo metoa wito kwa Watanzania kwa wale wenye Maeneo ya Uwekezaji waweze kwenda katika kituo Cha Uwekezaji hapa nchi TIc ili waweze kuwatafuta watu kuwekeza maeneo hayo.
Previous Post Next Post