Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limemkamata Gamariel Swai (43)mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi kwa tuhuma za kuuza spea za magari zilizoibwa kwenye magari ya watu mbalimbali .
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro, amesema mtuhumiwa huyo Duka lake lipo Mtaa wa Songea, Ilala.
Amsema Awali Jeshi la Polisi tarehe 23 Julai 2022 lilipokea taarifa ya wizi wa vifaa vya gari huko maeneo ya Kivule bombambili Ukonga ambapo Sifael Msemwa (38) mkazi wa. Bomba mbili aliibiwa vifaa vya gari yake aliyokuwa ameiegesha nyumbani kwake aina ya Toyota Prado yenye usajili namba. T. 429 BKK ambavyo ni side mirror 03, power window 04, control box na betri la gari.
"Tarehe 15 Agosti 2022 baada ya upelelezi alikamatwa mtuhumiwa Gama Swai na katika upekuzi katika duka lake Namba 21 lililopo mtaa wa Songea, Ilala alikutwa na side mirror 02 na power window 04 zilizoibwa toka katika gari hilo Toyota Prado"amesema kamanda Muliro
Aidha amesema vilikamatwa vifaa vingine mbalimbali vya magari dukani hapo vinavyo dhaniwa kuwa ni vya wizi kutokana na kuto kuwepo na maelezo ya kutosha kuhusiana na vifaa hivyo.
"Vitu vilivyokamatwa ni Taa za mbele 93 za magari ya aina mbalimbali, taa za nyuma 130 za
magari ya aina mbalimbali, power window 189 za magari ya aina mbalimbali, side mirror 62 za magari ya aina mbalimbali, show za mbele
za magari 07 mbalimbali, show za ndani za magari 35 za aina mbalimbali, mikono ya milango (vitasa) 26 za magari, rejeta 01 na betri moja" amsema kamanda Muliro.
Katika hatua nyingine Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalumya Dar es salaam limemkamata Maarifa Hadith Matala (45), Dereva wa daladala, mkazi wa Kimara Suka Golani Wilaya ya Ubungo kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake, Sharifa Twaha Nyamaishwa (31), Kondakta wa Daladala aliyekuwa mkazi wa Kimara Suka Golani Wilaya ya Ubungo kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili na kumuua, tukio hilo limetokea tarehe 16 Agosti 2022 huko maeneo ya Kimara Suka, na mara baada ya tuko
hilomtuhumiwa alitoweka.
Amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na oparasheni kali dhidi watu wanajihusisha na matukio ya kihalifu ikiwa ni pamoja wizi wa magari na uuzaji wa vifaa vya magari vitokanavyo na magari ya wizi.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro akionyesha Baadhi ya spea Magari za wizi ilizokutwa kwenye duka la Gamariel Swai (43) lilipo ilala jijini Dar es salaam.