MWENYEKITai wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema kuwa kosa la mtu mmoja lisisababishe chombo cha habari kufungiwa na kunyima haki ya wananchi kupata habari.
Balile ameyasema hayo leo Agosti 11 wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC), ambapo alikua akizungumzia vifungu vya sheria vitakavyokwenda kujadiliwa kati ya wadau wa habari na Serikali katika mkutano utakaofanyika leo Agosti 11 katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Balile amesema unakuta chombo cha habari kinajiendesha kwa misingi na maadili mazuri na kinafuata sheria lakini mtu binafsi au kiongozi anaenda kufanya mahojiano kweye kipindi fulani na anatoa maneno yasiyofaa ambayo yanasababisha chombo cha habari kufungiwa kwa hii sio sawa kabisa.
" Ni vyema mtu binafsi akawajibika na kubeba lawama sio chombo cha habari unapofungia chombo kwa kosa la mtu binafsi unawanyima wananchi kupata habari mfano kuna watu wameweka matangazo yao unadhani chombo kikifungiwa wao watafikia vipi lengo lao la kutangaza.
"Pia itasababisha wafanyakazi kama madereva , wapishi pia litasababisha hata wanafunzi kwenda kwenda kutokana haki kukosa kupata habari Kwa kosa la mtu mmoja.
'Kama Mwandishi akifanya ndivyo sivyo aadhibiwe kwanza kisha taratibu zingine za kufungua chombo cha habari zifuatwe," amesema.
Balile ameongeza kuwa ili chombo kiwajibishwe ni lazima ufanyike uchunguzi ili kujiridhisha kwamba chombo cha habari kimeunga mkono kilichofanywa na mtu binafsi ambaye amesabanisha kuleta taharuki kwenye jamii.
Kuhusu mapendekezo ya kiwango cha elimu kwenye taaluma ya uandishi wa habari Balile amesema TEF imependekeza kiwango cha awali iwe ni shahada ya kwanza ili kuipa heshima tasnia ya habari kama ilivyo kwa tasnia nyingine
" Ni aibu mtu kusimama na kusema mimi siendi kusoma , unakuta mtu akijua kusoma na kuandika tu na yeye anataka kuwa mwandishi wa habari hii sio sawa kama unaweza kusoma na kuandika basi aende uwanja wa ndege ukaombe apewe ndege arushe kama utaaweza Kwa kuelekezwa Tu kama itawezekana" amesisitiza.
Ameongeza kuwa kuna vifungu 16 kati ya vifungu 67 ambavyo wadau wa habari wanapiga Kelele kuomba kufanyiwa marekebisho kutokana na kumnyima haki mwandishi wa habari.